Waziri Afya, Jenista Mhagama: Ugonjwa wa kipindupindu umekuwa ukiwachukua Watu kutokana uchafu

informer 06

Member
Joined
May 11, 2024
Posts
66
Reaction score
49
Waziri wa Afya,Jenista Mhagama amezitaka jamii kuendelea kuchukua tahadhari ya magonjwa ya msimu ambayo yamekuwa yakiibuka kwa nyakati tofauti hususani ugonjwa wa kipindupindu ambao amedai umekuwa ukipelekea vifo.

Amesema kuwa ugonjwa wa Kipindupindu umekuwa ukiwachukuwa watu. Lakini ameeleza kwamba ugonjwa huo umekuwa ukisabishwa na uchafu.
IMG_0066.jpeg
Akizungumza leo January 3, 2025 akiwa katika hospitali ya Mkoa wa Kagera iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Mhagama ameyataja magonjwa mengine kama Corona, Ugonjwa wa virusi vya Marburg pamoja na mengine.

Katika kuchukua hatua za kukabiliana na athari za magonjwa hayo amesema kwamba Serikali ipo katika mpango wa ujenzi wa hospitali maalumu mkoani Kagera kwa ajili ya magonjwa ya mlipuko.

"Pamoja na jambo la maalumu la wahudumu wa afya ngazi ya jamii lakini mimefanya kazi kukagua mpango wa Serikali, azima ya Serikali, nia ya Serikali ya kuwa na Hospitali maalumu kwa ajili ya magonjwa ya mlipuko katika Mkoa wetu wa Kagera"amesema
IMG_0068.jpeg
Lakini amebainisha jitihada nyingine kwamba ni kutoa nguvu kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii ambao wanaendelea kupatiwa mafuzo kwa ajili ya kuanza kuhudumia jamii, amesema kuwa wahudumu hao wataenda kuongeza nguvu ya katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiafya ambazo zinakumba jamii.

Aidha amesema kwamba wahudumu hao wanajengewa uwezo wa kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kushauri, kufanya vipimo kwa baadhi magonjwa pamoja na kubaini viashiria vya magonjwa na kuchukua hatua stahiki mapema.
IMG_0080.jpeg
Licha ya hivyo amewahasa wahudumu kuzingatia miiko ya kazi ikiwemo kutunza siri za watu wanaowahudumia, ambapo amesisitiza kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaoenda kinyume na miiko ikiwemo suala hilo la kutunza siri.
 
Kipindupindu hakitaisha kwenye jamii zetu kwa sababu ya uchafu na utupaji hovyo wa taka.
Miji mingi bado mifumo ya uchakataji wa maji taka haipo. Mfano kipindi cha mvua kwenye baadhi miji kuna watu hufungulia au humwaga maji taka na kila aina ya uchafu kwenye mifereji ya mvua ndiyo maana tunashuhudia milipuko ya magonjwa kama kipindupindu.

Atakayetuokoa hakuna, bali ni sisi wenyewe kuamka na kuchukua hatua kwa kukemea wale tunaowashuhudia wakimwaga taka/uchafu hovyo na si kuwasubiri wanasiasa....
 
Amesahau shida kubwa ni umasikini uliosababishwa na CCM.

Uchafu na umasikini vinaendana, umasikini wa kipato, umasikini wa akili vyote hivyo huleta kipindupindu.

Boresheni maisha ya watu na kujenga miundo mbinu Bora muone kama kipindupindu kitakuwepo.

Mbona Kuwait, Qatar, USA, UK ,Germany, Finland, France nk hakuna kipindupindu.
 
Back
Top Bottom