Waziri Akwilapo atoa onyo kali kwa wavamizi wa ardhi

Waziri Akwilapo atoa onyo kali kwa wavamizi wa ardhi

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165
23166ed9-6035-4b45-a7cd-6a6b9a1f14e3.jpeg

DAR ES SALAAM- Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo, amewaonya wananchi wanaovamia maeneo kwa nguvu na kuunda vikosi vya ulinzi kwa ajili ya kulinda maeneo hayo, akisema Serikali haitavumilia vitendo hivyo na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Dkt. Akwilapo ametoa onyo hilo leo Sept 17, 2026 wakati akizungumza na wananchi katika Kliniki ya Ardhi iliyofanyika Kata ya Zingiziwa, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Amesema, wananchi hawapaswi kujichukulia sheria mkononi kwa kuvamia maeneo yanayomilikiwa na watu wengine na kuanzisha vikosi vya ulinzi kwa lengo la kuyadhibiti kwa nguvu.

“Serikali haitavumilia vitendo vya watu kujichukulia sheria kwa kuvamia maeneo ya wananchi wengine na kuunda vikosi vya ulinzi kwa lengo la kulinda maeneo hayo kwa nguvu,” amesema Dkt. Akwilapo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Bw. Elihuruma Mabelya, amesema hadi sasa jumla ya hati miliki 545 zimetolewa kwa wananchi kupitia Kliniki hiyo ya Ardhi.

Mabelya ameeleza kuwa, timu ya wataalamu itaendelea kuwepo katika eneo hilo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za ardhi kwa urahisi na kwa wakati, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Wizara.

Baadhi ya wananchi, kupitia Diwani wa Kata hiyo, wameipongeza Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kusogeza huduma za ardhi karibu na maeneo yao.

Wameielezea hatua hiyo kuwa imewapunguzia adha ya kusafiri umbali mrefu pamoja na gharama kubwa walizokuwa wakitumia ili kufuata huduma hizo.
 
Hii sector ya Ardhi imeoza imeoza haina hata maana.
 
📌📌📌

Due to government corruption in Tanzania, most land grabbing is in fact sponsored by government officials.

The inefficiency of the government in dealing with land disputes (it taking even several decades to solve a land dispute) is also what is leading to increasing levels of vigilantism.

Law and order is hard to maintain when those trusted to protect and facilitate it are the first ones to engage in breaking laws.

It is distressing to see that most land disputes in Tanzania remain unresolved.
 
Back
Top Bottom