Waziri aonya watendaji RUWASA kuchafuana wakisaka madaraka, ataka watoe huduma bora kwa wananchi

Waziri aonya watendaji RUWASA kuchafuana wakisaka madaraka, ataka watoe huduma bora kwa wananchi

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi amewaonya watendaji wa Mamlaka ya Maji Vijini (RUWASA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, akiwataka kuacha mara moja tabia ya kuchafuana kwa lengo la kusaka madaraka.

Amewataka wafanye kazi kwa pamoja kuhakikisha miradi ya maji inayotekelezwa na Serikali kwenye maeneo yao inakamilika kwa wakati na wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama.

Mhandisi Maryprisca Mahundi ametoa onyo hilo wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mkula wilayani Busega wakati akikagua mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni mbili unaotekelezwa na Serikali kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa vijiji vitano vya eneo hilo.

Amewataka watendaji hao kuanza kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta tija na kudai kuwa tabia ya kuchafuana itasababisha halmashauri hiyo kuwapoteza viongozi wenye uwezo wa kuwasaidia wananchi kupata maji.


Source: Malunde

IMG-20220303-WA0003.jpg
 
Wanafuata nyayo zao wanasiasa, kwa siku hizi kuchafuana ndio kunaleta vyeo.
 
Back
Top Bottom