Waziri asema kiwango cha udumavu kwa Watoto Mkoani Iringa ni 47%

Waziri asema kiwango cha udumavu kwa Watoto Mkoani Iringa ni 47%

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Waziri wa Afya, Waziri Ummy Mwalimu amesema katika Mkoa wa Iringa kuna tatizo kubwa la udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Ameyasema hayo leo Agosti 13, 2022 akidai kuwa kiwango cha udumavu mkoani humo ni asilimia 47 ambapo katika kila watoto 100, watoto 47 wamedumaa.

“Tunazungumzia kuboresha elimu, afya, miundombinu na vingine vingi lakini kama watoto wamedumaa hawawezi kufundishika hatutakuwa madaktari, walimu wahandisi wazuri.

“Tunapovua samaki tusiuze wote tuwape watoto wetu, tunywe maziwa tutapunguza watoto wanaoumwa hovyo,” - Ummy Mwalimu.
 
Nimeshiriki sana vikao vya lishe. Hizi takwimu si za kuaminika sana kwani wanaondaa takwimu ni wale wanaosimamia mradi wa Lishe. Ikionekana udumavu umepungua basi wafadhali watasitisha kutoa fedha. Hivyo inabidi ionekane kuwa ipo juu.
 
Back
Top Bottom