Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa wa fedha katika sekta ya maji katika Jiji la Mwanza kwani miradi mingi inaendelea na ikikamilika changamoto ya maji itategemewa kubaki historia.
Waziri Aweso ameyasema hayo tarehe 21 Desemba 2024 wakati Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa alipotembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Tanki la Kuhifadhi Majisafi Kisesa- Bujora Mwanza.
Katika hatua nyingine, Waziri Aweso amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) kwa kuondoa malalamiko ya mara kwa mara ya ukosefu na upungufu wa huduma ya maji Mwanza na viunga vyake.
Waziri Aweso amekiri kwamba kulikuwa na malalamiko makubwa kuhusu upatikanaji wa maji ila kwa sasa yamepungua tangu Mkurugenzi Nelly Msuya aanze kazi.