Waziri Aweso atii agizo la Rais Samia, afika Kwamsisi Tanga

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Waziri wa Maji Jumaa Aweso amefika kijiji cha Kwamsisi kilichopo katika kata ya Kwamsisi, wilayani Handeni mkoani Tanga kujionea hali ya upatikanaji wa maji katika eneo hilo na changamoto iliyobainika kutokana na video iliyochapishwa katika ukurasa wa Instagram wa mtangazaji Mbarouk Khan.

Mbarouk alichapisha video inayoonesha changamoto ya maji kwa wakazi wa eneo hilo huku akieledha adha wanayoipata kutokana na changamoto hiyo, hali iliyomgusa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alimtaka Waziri Aweso ahakikishe changamoto ya upatikanaji wa maji safi katika eneo hilo inatatuliwa.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…