Waziri Aweso: Maji yapo, aagiza wafanyakazi wa DAWASA kutokaa ofisini "Wananchi wanahitaji maji"

 Waziri Aweso: Maji yapo, aagiza wafanyakazi wa DAWASA kutokaa ofisini "Wananchi wanahitaji maji"

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
WaziriI wa Maji, Jumaa Aweso amewahakikishia wakazi wa Dar es Salaam na Pwani, upatikanaji wa maji safi na salama katika mikoa hiyo kwani changamoto ya hitilafu ya mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu juu tayari imerekebishwa.

Waziri Aweso ameyasema hayo leo Oktoba 28, 2024 katika ziara ya kukagua na kutembelea mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Juu na kujione mwenyewe ukarabati uliofanywa na wahandishi wa Dawasa baada ya kutokea kwa hitilafu katika moja ya mitambo kiasi cha kuathiri uzalishaji wa maji safi na salama.

===

1.AWESO: DAWASA MSIKAE OFISINI, WANANCHI WANAHITAJI MAJI

2.AWESO AWAHAKIKISHIA UPATIKANAJI WA MAJI DAR NA PWANI
3."MAJI HAYANA MBADALA, TUNAFANYA KILA TUWEZALO KUWAPA HUDUMA" AWESO

NA Mwandishi Wetu, Pwani
Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso amewahakikishia wakazi wa Dar es Salaam na Pwani upatikanaji wa maji safi na salama katika mikoa hiyo kwani Changamoto ya hitilafu ya mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu juu tayari imerekebishwa.

Waziri Aweso ameyasema haya leo Oktoba 28, 2024 katika ziara ya kukagua na kutembelea mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Juu na kujione mwenyewe ukarabati uliofanywa na wahandishi wa Dawasa baada ya kutokea kwa hitilafu katika moja ya mitambo kiasi cha kuathiri uzalishaji wa maji safi na salama.

Amesema kwa kawaida mtambo wa Ruvu juu ukiwa katika hali ya ubora wake unazalisha maji kiasi cha lita 197milioni kwa siku , lakini baada ya kutokea kwa hitilafu uzalishaji wa maji ulikuwa katika kiwango cha chini kiasi cha lita 170milioni hivyo kuathiri upatikanaji wa maji katika maeneo hayo.

"Nilikuwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu nikapata taarifa za kelele za malalamiko kuhusu kukosekana kwa maji hasa katika maeneo ya malamba mawili, Saranga, Mbezi Msakuzi, Bonyokwa na maeneo mengine nikalazimika kumaliza ziara ili nije nijue tatizo ni nini" amesema Aweso.

Waziri Awezo amesema anawashukuru mafundi kutoka Dawasa kwani walihakikisha kuwa wanafanya kazi usiku na mchana kumaliza tatizo hilo ili wananchi waendelee kuifurahia huduma ya maji jambo ambalo tayari limeshapatiwa ufumbuzi.

"Niwahakikishie ndugu zangu wananchi, upatikanaji wa maji kwa sasa umerudi katika hali yake, mafundi wetu wameshafanya kazi usiku na mchana kumaliza tatizo hilo."amesema Waziri Aweso.

Aidha ametoa agizo kwa wafanyakazi wa Dawasa pamoja na Wizara yake kuhakikisha kuwa hawazizoei shida za wananchi bali wahakikishe kuwa wanawapatia maji safi na salama kwa wakati kwani wakazi wa Pwani na Dar es Salaam hawana mbadala mwingine wa maji.

"Menejimenti msikae ofisini, maji hayana mbadala hivyo Dawasa timizeni wajibu wenu, hatuna kisingizio kwamba maji katika mto yapo kidogo, maji yapo ya kutosha, tuwaombe wananchi radhi kwa hii hitilafu, piteni maeneo yote tusilete visingizio:" Amesema Waziri Aweso.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon pamoja na kumshukuru waziri Aweso kutembelea katika mtambo huo amesema kwa sasa wamewekeza zaidi katika kuhakikisha kuwa mifugo haiathiri vyanzo vya maji na maji yanaendelea kutiririka kama kawaida.

Amesema siku za karibuni wameondoa zaidi ya ng'ombe 3000 katika mto Ruvu lengo likiwa ni kukilinda chanzo hicho cha maji ili maji yaendelee kutiririka na wananchi waweze kupata maji safi na salama.

"Tumeimarisha ulinzi kwenye mto wetu wa Ruvu, juzi tuliondoa zaidi ya mifugo 3000 na tayari tumeshaandaa vyanzo vingine vya kunywesha maji mifugo yetu, lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wa Dar es Salaam na Pwani wanaendelea kupata maji safi na Salama." amesema DC Nickson.

Mkuu wa Wilaya Nickson amesema chanzo mama cha upatikanaji wa maji kitaendelea kulindwa kwa wivu mkubwa hasa katika kipindi hiki cha ukame, mvua zikisubiriwa tena kujaza mito na vyanzo vingine vya maji.

Hata hivyo Katibu wa siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani David Mramba amesema wiki mbili zilizopita Wizara ya maji ilituma wataalamu wake baada ya kutokea kwa hitilafu katika mtambo wa Ruvu Juu.

Amesema wataalamu hao na mafundi walifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kuwa wanamaliza tatizo hilo ili wananchi wa Pwani na Dar es Salaam wanaendelea kufurahia huduma ya maji safi na salama

Soma, Pia:

Waziri Aweso akutana na DAWASA kwa lengo la kuboresha huduma ya maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani

Jumaa Aweso: Maji yapo, umeme upo, ni marufuku kutoa Maji Saa Nane Usiku

KERO - CCM na serikali yenu kuandikisha watoto wawapigie kura mnaweza, ila kuhakikisha tunapata huduma za muhimu kama maji Aaaaa!
 
Wakuu

Wakati wa wakazi wa Dar wakiwa wanaendelea kulalamika kuhusu kero ya maji. Waziri wa Maji, Mhe. Juma Aweso, amejitokeza hivi karibuni na kuwahakikishia wakazi wa Dar es Salaam na Pwani maji safi na salama yapo na yataendelea kupatikana.

Aweso alifanya ziara katika mtambo huo, ambapo alibaini kuwa uzalishaji wa maji umerejea kwenye kiwango cha kawaida cha lita milioni 197 kwa siku na kuwahakikishia wakazi wa Pwani na Dar kuwa wako vizuri.

Soma pia: Waziri Aweso: Maji yapo, aagiza wafanyakazi wa DAWASA kutokaa ofisini "Wananchi wanahitaji maji"

VIpi wewe mtaani kwako mkuu, haya maji yapo kama anavyotuambia Waziri au ndio talking points za CCM?



 
Wakuu,

Inaonekana kuna mazingira yanaandaliwa na hawa viongozi kuonesha kuwa wanafanya sana kazi hasa katika kipindi hiki ambacho Taifa linaeleka kwenye Ucahguzi

Siku ya jana Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, alifanya ziara majira ya usiku akikagua hali ya upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.

Kuna umuhimu gani wa kukagua miradi usiku lakini? Mchana wote walikuwa wapi?

Tunajua mnajaribu kufanya spinning na kutaka kuonesha kuwa mnastahili teuzi zijazo lakini mnaiweka too obvious.


 
Mwanzoni aliingia na gia kali sana Watu wakajua wamepata jembe kumbeee with time ikaanza kuonekana kana kwamba ilikuwa nguvu ya soda tu.
 
Wakuu,

Inaonekana kuna mazingira yanaandaliwa na hawa viongozi kuonesha kuwa wanafanya sana kazi hasa katika kipindi hiki ambacho Taifa linaeleka kwenye Ucahguzi

Siku ya jana Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, alifanya ziara majira ya usiku akikagua hali ya upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.

Kuna umuhimu gani wa kukagua miradi usiku lakini? Mchana wote walikuwa wapi?

Tunajua mnajaribu kufanya spinning na kutaka kuonesha kuwa mnastahili teuzi zijazo lakini mnaiweka too obvious.


Kazi mda wote.
 
Tatizo la maji Dar linahita ukaguzi wa raslimali watu mitambo na vifaa pamoja na miundombu ya huduma ya maji.Si jambo la kuwamini wanasiasa tena kwani hata wao hawajui kwanini maji yakosekane
 
Back
Top Bottom