Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana Ateta na Wajumbe wa Benki ya Dunia

Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana Ateta na Wajumbe wa Benki ya Dunia

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WAZIRI BALOZI DKT. PINDI CHANA ATETA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Benki ya Dunia ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii, jijini Dodoma leo Septemba 5, 2024.

Ujumbe huo umekuja kumpatia mrejesho wa ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Benki ya Dunia hasa katika uhifadhi wa maliasili na utekelezaji wa mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW)ikizingatiwa kwamba Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) ameteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuiongoza Wizara hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Chana ameishukuru Benki ya Dunia kwa namna ambavyo imeendelea kuiwezesha Tanzania kwenye juhudi zake za uhifadhi na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshugulikia maliasili, Kamishna Benedict Wakulyamba na Mratibu wa Mradi wa REGROW, Aenea Saanya.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-09-06 at 14.40.21.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-06 at 14.40.21.jpeg
    371.9 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-09-06 at 14.40.22.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-06 at 14.40.22.jpeg
    416.8 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-09-06 at 14.40.22(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-06 at 14.40.22(1).jpeg
    352.4 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-09-06 at 14.40.23.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-06 at 14.40.23.jpeg
    265.5 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-09-06 at 14.40.23(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-06 at 14.40.23(1).jpeg
    215.7 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-09-06 at 14.40.24.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-06 at 14.40.24.jpeg
    232.4 KB · Views: 3
Back
Top Bottom