Unapozungumzia "Quality" hapo unazungumzia Soko!!
Unapozungumzia "Quantity" hapo unazungumzia Soko!!
Na unapozungumzia "Consistence" Pia unazungumzia Soko.
Hebu tulijadili kidogo.
Unapozungumzia Ubora wa mazao moja kwa moja unazungumzia kupeleka mazao hayo kwa mteja ama kuyashindanisha na ya mwengine sokoni yakiwa na ubora unaotakiwa. Sidhani unazungumzia ubora kwa ajil ya mazao ya kutumia kwenye familia.
Tukija kwenye suala la wingi nalo ni vile vile. Inawezekana kabisa kuna hisia kwamba Tanzania tunazalisha mazao yasiyo na ubora na machache yasiyotosheleza soko. Kwa ivo unaposema tatizo la Kilimo chetu ni uchache wa mazao tunayozalisha upo sahihi, lakini hapo bado unazungumzia soko.
Na pale unapozungumzia Muendelezo, ni kwamba umeunganisha mambo mawili ya mwanzo, yaani Ubora na wingi na kuyaweka yawe ni kitu cha kudumu. Unapozungumzia uendelevu bado pia unazungumzia Soko. Yaani kutu kinachouzwa leo kiuzwe kesho kikiwa na ubora na wingi ule ule.
Sasa hapo ndiyo ujue hayo matatizo ya kutokuwa na "Quality, Quantity, Consistence" ndiyo mkulima anayosumbuliwa nayo hatimaye mazao yake yanakosa soko.
Lakini kwa Tanzania hizo zinazoitwa "Program" huwa zimejaa nadharia zaidi kuliko uhalisia na wala huwa siyo suluhu kudumu kwa matatizo yetu kwenye Kilimo. Hao waliomo kwenye hiyo BBT ni wakulima maskini waliotolewa vijijini ama ni vijana wapya wa kisiasa wanaopelekwa kutumia hizo fedha kwenye jaribio la kilimo lisilo la kisayansi??