Bongo movie tu hiyoHii nchi ngumu Sana siasa zimejaa Kila mahali Hawa vijana waliotafutwa wamjini hawajui hata kushika jembe ndio wanategemewa kizalisha mazao kweli? Wacha muda utasema
Sent from my RMX2189 using JamiiForums mobile app
Kaka Allen, soko la mazao sio tatizo kabisa, tatizo ni "QQC" (quality, quantity and consistence ya mazao yetu). Hatuzalishi mazao katika ubora na wingi unaowezesha economies of scale itokee na mwendelezo wa hicho kinachozalishwa na hivyo kutoa nafasi ya kutwaa soko la kimataifa.Tanzania tatizo la kilimo ni moja tu. SOKO LA MAZAO YA WAKULIMA.
Unapozungumzia "Quality" hapo unazungumzia Soko!!Kaka Allen, soko la mazao sio tatizo kabisa, tatizo ni "QQC" (quality, quantity and consistence ya mazao yetu).
Kwani amesema watalima kwa kutumia majembe? I hope ni matrektaHii nchi ngumu Sana siasa zimejaa Kila mahali Hawa vijana waliotafutwa wamjini hawajui hata kushika jembe ndio wanategemewa kizalisha mazao kweli? Wacha muda utasema
Sent from my RMX2189 using JamiiForums mobile app
Sikia walioandaa andiko la BBT project!Ni mara ngapi tumeona clip na picha zikionesha wakulima wakilia kwa kukosa masoko ya mazao yao.
*Tushaona nyanya zinauzwa debe sh 500/= na parachichi zikioza huko Iringa.
*Tushaona mahindi yakioza huko Songea na Katavi.
*Tushaona wakulima wa korosho wakiuza korosho kwa bei ya hasara ama kugomea masoko huko Mtwara.
*Tushaona wakulima wakikata mibuni na michai kwa bei mbaya ya mazao hayo.
Kilimo kimeshindwa kuvutia vijana kwasabb 2 tu.
1. Kukosekana kwa masoko ya uhakika ya kumfanya mkulima apate faida (sababu kubwa zaidi hii)
2. Upatikqnaji wa uhakika wa pembejeo na viwatilifu.
Kama wakulima wangekuwa wanapata faida hakuna kijana angekuwa bodaboda, machinga ama mamantilie. Wote wangejikita kwenye kilimo. Shughuli yoyote ya kiuchumi yenye faida huvutia watu.
Kwahiyo siyo kwamba vijana hawataki kilimo kwasbb ya ukosefu wa mitaji....NO.
Nani alitoa mafunzo na mitaji kwa bodaboda, mamantilie na machinga waliozagaa nchi nzima?
Wasomi wa SUA waliomaliza miaka dahali pamoja na maprofesa wao mbana hatuoni wakitumia utaalamu wao kuendesha mashamba makubwa??
Bashe ktk hili unatapanaya tu hela zetu za Kodi lkn zoezi la BBT halitafanikiwa wala halitakuwa endelevu. Kilimo hakiendeshwi hivyo.
Kazi ya serikali kupitia wizara ya kilimo iwe ni kujenga mifumo itakayoifanya shughuli ya kilimo kwenda sawa na kuvutia watu wengi zaidi.
NIMEMALIZA.
Kilimo cha selfie hiki hakifiki popoteHii nchi ngumu Sana siasa zimejaa Kila mahali Hawa vijana waliotafutwa wamjini hawajui hata kushika jembe ndio wanategemewa kizalisha mazao kweli? Wacha muda utasema
Sent from my RMX2189 using JamiiForums mobile app
Hahaha! Daah!Sikia walioandaa andiko la BBT project!View attachment 2565376
Yaani "Buying power" ndiyo huamua soko. Unaposema "SOKO" ni neno linalobeba mkurulo mzima wa biashara ya mazao na kurudi kinyume nyume mpaka kwa mzalishaji!!Tatizo ni Soko na watu hawana buying power;
Mwandishi wa andiko ktk ubora wako. Sasa kwann wizara isiweke nguvu ktk kuondoa hizo changamoto kwa wakulima badala yake inaanzisha BBT?Kaka Allen, soko la mazao sio tatizo kabisa, tatizo ni "QQC" (quality, quantity and consistence ya mazao yetu). Hatuzalishi mazao katika ubora na wingi unaowezesha economies of scale itokee na mwendelezo wa hicho kinachozalishwa na hivyo kutoa nafasi ya kutwaa soko la kimataifa. Huwezi kuwalisha watu mchele kwa msimu. Ima uzalishe mara 3-4 kwa msimu au uzalishe kwa msimu mmoja lakini kwa kiwango kikubwa chenye kutosheleza mahitaji ya mwaka mzima. Program ya BBT ni best program ever katika nchi yetu as long uzalishaji ukifanyika bila kutegeme mvua na kwa wingi kukidhi mahitaji ya containers (sio gunia).
Bonge moja la hoja. Kongole mkuuUnapozungumzia "Quality" hapo unazungumzia Soko!!
Unapozungumzia "Quantity" hapo unazungumzia Soko!!
Na unapozungumzia "Consistence" Pia unazungumzia Soko.
Hebu tulijadili kidogo.
Unapozungumzia Ubora wa mazao moja kwa moja unazungumzia kupeleka mazao hayo kwa mteja ama kuyashindanisha na ya mwengine sokoni yakiwa na ubora unaotakiwa. Sidhani unazungumzia ubora kwa ajil ya mazao ya kutumia kwenye familia.
Tukija kwenye suala la wingi nalo ni vile vile. Inawezekana kabisa kuna hisia kwamba Tanzania tunazalisha mazao yasiyo na ubora na machache yasiyotosheleza soko. Kwa ivo unaposema tatizo la Kilimo chetu ni uchache wa mazao tunayozalisha upo sahihi, lakini hapo bado unazungumzia soko.
Na pale unapozungumzia Muendelezo, ni kwamba umeunganisha mambo mawili ya mwanzo, yaani Ubora na wingi na kuyaweka yawe ni kitu cha kudumu. Unapozungumzia uendelevu bado pia unazungumzia Soko. Yaani kutu kinachouzwa leo kiuzwe kesho kikiwa na ubora na wingi ule ule.
Sasa hapo ndiyo ujue hayo matatizo ya kutokuwa na "Quality, Quantity, Consistence" ndiyo mkulima anayosumbuliwa nayo hatimaye mazao yake yanakosa soko.
Lakini kwa Tanzania hizo zinazoitwa "Program" huwa zimejaa nadharia zaidi kuliko uhalisia na wala huwa siyo suluhu kudumu kwa matatizo yetu kwenye Kilimo. Hao waliomo kwenye hiyo BBT ni wakulima maskini waliotolewa vijijini ama ni vijana wapya wa kisiasa wanaopelekwa kutumia hizo fedha kwenye jaribio la kilimo lisilo la kisayansi??
Kwa ligha nyepesi mwambie "SOKO ni f(Quantity, Quality & Consistency)Yaani "Buying power" ndiyo huamua soko. Unaposema "SOKO" ni neno linalobeba mkurulo mzima wa biashara ya mazao na kurudi kinyume nyume mpaka kwa mzalishaji!!
Watu wanaweza wakawa wana uwezo wa kununua lakini unauza makapi no one wants it; au wanaweza wakawa wanataka hio product yako lakini uwezo wa kununua hakuna.....Yaani "Buying power" ndiyo huamua soko. Unaposema "SOKO" ni neno linalobeba mkurulo mzima wa biashara ya mazao na kurudi kinyume nyume mpaka kwa mzalishaji!!
Kabisa kabisa! Wakulima wanalazimika kuwauzia walanguzi huko mashambani kwa bei yeyote ile ndogo kwa sababu wanaogopa kuyapeleka sokoni kwa kuwa huko ndio kuna usumbufu mkubwa sana kwa madalali na hata mazao yanaweza yakaharibika akijifanya mjuaji !! Ni kweli shida kubwa ni masoko ambayo hayatakuwa na janja janja za kumpunja mkulima !Tanzania tatizo la kilimo ni moja tu. SOKO LA MAZAO YA WAKULIMA.
Serikali inapaswa ije na mfumo ambao automatically utawatoa madalali kwenye mfumo. Hii itakuwa ahuen kwa mkulimaTatizo sio dalali bali ni mifumo mibovu tu.kwani kama kuna mifumo mizuri huyo dalali atatokea wapi?!!
Ohoooo!Bila kutengeneza miradi ya mchongo utapigaje pesa