Waziri Bashe hakutakiwa kuukataa msaada wa mchele kutoka Marekani na kama alikuwa na mashaka yoyote angewatumia TBS

Sio kwamba alikua hajui sema ni kwakua lime bumbuluka ivyo kaona apite na upepo wa siasa ... na sio kwamba mchele auta letwa .mchele uta kuja kama kawaidaaa na hamna kitu mta fanya
 
Kama Kuna shule 10 na kati ya hizo shule Moja ina uhitaji mkubwa sana wa walimu na vifaa vya kufundishia kuliko zingine, ukitaka kupeleka walimu utaanza na zipi?
Kuna watu wanauliza maswali ya kijinga sana.
 
Ukiambiwa wananunua mchele kilo 200 mtauza? Maana inawezekana kwao wananunua kilo shs 200
Kilo miambili, mifuko kuprint, kuinunua, kusafirisha mpaka kwa mlengwa hata tz unafikiri ni gharama ndogo?

Vya bure vyaua , hivi huo mchele wa kuuziwa kilo mia 200, huo ni mchele au makapi
 
Yani unahitaji mafunzo ya kulima mchele wakati tayari ushapigwa na njaa hiyo ni ngumu ukweli ni kwamba Tanzania tunajisifia tu kwamba tunachakula cha kutosha ila hakuna wanafunzi wanakunywa uji familia nyingi zinaishi kwa kula mlo mmoja mpaka miwili tena isiyo kamili...
 
Lengo la msaada likiwa zuri hakuna sababu ya kukataa msaada, dunia nzima wanaishi hivyo
Sio kweli kwamba wamekaataa hizi ni mboyoyo tu za kwenye kipaza ila mchele utatumiwa na watauiba wataungiza sokoni wapate pesa kabisa
 
Ninachojiuliza, kwani tz kuna njaa. Nani alieomba huo msaada. Wa Tz kupenda kitonga hawajanbo
 
Hawa wazalendo uchwara wanachosha sana na kelele zao.
 
Wamarekani ni binadamu wenye utu na uchungu na raia wa nchii hii. Wao wanajua kwamba raia wana shida na njaa na viongozi hawajali. Wao wanajua kuwa viongozi wanaishi kwenye maisha ya kifahari ila raia wanakufa kwa njaa. Wanafanya haya kwa sababu wanajali maisha ya watanzania na siyo kama kina Bashe. Bashe hata wafe raia elfu hana uchungu wowote. Unakumbuka kipindi cha Magufuli ilikuwa marufuku kusema sehemu fulani inakabiliwa na njaa hata kama ilikuwa ni kweli?
 
Hawa wazalendo uchwara wanachosha sana na kelele zao.
Ndomana hatuendelei mana siasa kwenye kila kitu kama umepewa kitu si unajiridhisha kitaalamu si mnao wakemia na maabara kwann msifanye vipimo kujua usalama wa hicho chakula kabla ya kuanza kutafuta kiki kwa raiya wenye njaa.
 
Unataka Wamarekani wakulishie shule zako zote juu ya kukujengea matundu ya vyoo pia??
Una evidence ya write up ya Serikali ya Tanzania kuomba msaada wa chakula kulisha hizo shule au ni janjajanja ya NGOs kushirikiana na US Dept of Agriculture kwa maslahi yao?! Wakitumia loopholes ya viongozi crooks hapa nchini? Watoto wetu wasitumike kama objects za kutajirisha wenye NGOs na wakulima wa marekani.
Bwashe yupo sahihi.
 

Hana ubavu wa kuzuia lolote 🀣🀣🀣🀣🀣
 
Kwani huo misaada ni wa serikali ya Marekani,au NGO kutoka Marekani? Acheni kubabaisha watu bhana,na hata kama tutapata Janga,sio Marekani tu itatusaidia,nyinyi kama mlikuwa na lengo la upigaji mmeliwa mtulie tu🀣🀣🀣
Kweli mnahitaji msaada au mnataka mpewe mkauze Burundi?
Nyie ndio wapiga dili mnapambana mpate magunia kadhaa mkayauze
Tunajua hata maturubali ya shirika la ukimbizi yalikuwa yanaibiwa Ulyankulu na kuuzwa kwa kuanikia mahindi badala ya tent au ulikuwa hujazaliwa?

Hamuhitaji misaada bali akili ya kujikomboa kutoka kwenye umasikini
Umasikini ni Laana
 
Watoto wenu wapeni ubwabwa mashuleni, acheni porojo za kwamba mchele mnao mwingi huku wao wakisoma na njaa na hata huo ubwabwa wa maharage bado ni anasa kwao.
 
Lengo la msaada likiwa zuri hakuna sababu ya kukataa msaada, dunia nzima wanaishi hivyo
"Virutubisho" kwenye huo mchele na maharage husika ndo vinatiliwa mashaka mkuu. Bora kuzuia kuliko kutibu.
Hao watoto wakila wakageuka "mabwabwa" tiba itapatikana?!
 
Watoto wenu wapeni ubwabwa mashuleni, acheni porojo za kwamba mchele mnao mwingi huku wao wakisoma na njaa na hata huo ubwabwa wa maharage bado ni anasa kwao.
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…........Wacha fujo chifu. Ubwabwa siyo tatizo kwenye shule zetu hapa nchini. Atleast mara 2 kwa wiki.
 
Ndomana hatuendelei mana siasa kwenye kila kitu kama umepewa kitu si unajiridhisha kitaalamu si mnao wakemia na maabara kwann msifanye vipimo kujua usalama wa hicho chakula kabla ya kuanza kutafuta kiki kwa raiya wenye njaa.
Hii ndio hoja yangu. Kuna TBS na mengine mengi ila hayatumiki
 
hajakataa ila nilichomuelewa ni kwamba fedha ambazo wanawalipa hao wakulima wao basi wangetupatia sie ili tujisaidie kwa kuwapa wakulima wetu ili kukuza kilimo nchini mwetu na inshu ya virutubisho wangekuja kuweka wenyewe hapa.

hakuna msaada wa bure,msaada una masharti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…