Waziri Bashe: Tuko kwenye hatua ya mwanzo ya mradi wa kesho imara

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
WAZIRI BASHE: TUKO KWENYE HATUA YA MWANZO YA MRADI WA KESHO IMARA.

"Nataka kukufahamisha kuhusu ‘Building a better tomorrow’ project Mradi huu uliopo hatua za mwanzo sisi wizara tutatenga fedha, kima cha chini 5B kwa kuanzia.

Kwasababu: Vijana hawaendi shambani na hawana motisha kuingia katika kilimo, changamoto za;
1) Upatikanaji wa Mtaji fedha
2) Upatikanaji wa Ardhi
3) Teknolojia
4) Masoko ya uhakika

Manbo haya yote huwakwamisha vijana na watanzania wengi wenye ndoto za kufanya kilimo Kikubwa na chenye tija.

Kwahivyo tumeamua kutengeneza maeneo Maalum ya kilimo (agricultural parks), maeneo haya yatafanyiwa vipimo (soil analysis etc) na upembuzi. Pia tutapeleka miundombinu ya maji na barabara. Baada ya kuweka vyote tutakata vipande shamba (block farms) ambazo tutawakabidhi vijana ambao watapatikana kwa programu maalumu yenye vigezo vya kukidhi.

Rai yangu kwa wadau wa maendeleo tutawafuata kuwaomba fedha tuchange pamoja.

Na lengo letu la msingi ni kuwapatia vijana mitaji hai na yenye tija. Kuanzia kwenye ardhi ambako tutaweka mifumo imara ya umwangiliaji, kuwafunda ukulima bora, tutawasaidia mbegu bora na mbolea ili wazalishe.

Hata hivyo tutawaunganisha vijana hawa na masoko kwajili ya mazao yao.

Jambo la msingi kwakua nia yetu na jambo hili lina tija kubwa hivyo Ardhi na fedha zote tutazitenga, na tutahakikisha tunawasaidia vijana hawa kutumia teknolojia za kisasa na mashine za kisasa za kilimo huku maeneo yote yakiunganishwa na mifumo rasmi ya wanunuzi (Offtakers).

Kwa kuwa na kilimo cha kisasa katika nchinyetu tutaongeza sio tu uzalishaji na ubora wa mazao yetu ili tutapunguza tatizo la ajira, tutahamasisha ushiriki wa vijana wengi kwenye kilimo na kujenga Uchumi endelevu wa nchi yetu."
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe

Screenshot_20220202-144758.jpg
 
Mimi huwa namkubali sana huyu dogo.
 
Vijana wanataka leo imara. Kesho kesho inaleta njaa.
 
Tunashindwa kuelewa hili kilimo cha Kisasa kiwe cha Kisasa kweli hakiitaji large numbers (huko kwenye kulima ni machinery tu) labda watu huku kwenye value addition....

Pili hao vijana wakishapewa blocks input yao ni ipi ? hizo mashine wanalimiwa ?, wanakodi mashine au wanagawana faida, Na hio faida ikigawanywa kwa wengi bado produce itakuwa ya gharama nafuu hadi kupelekea ku-compete kwenye soko la kidunia ?

Ni changamoto ipo na utatuzi wake utahitaji sana muunganiko wa nguvu kutoka sehemu tofauti; Ushauri kwanza waanze na masoko kutafutia hawa ambao tayari wana produce alafu tuendelee na hiyo michakato ya uzalishaji zaidi na wenye tija
 
WAZIRI BASHE: TUKO KWENYE HATUA YA MWANZO YA MRADI WA KESHO IMARA.

"Nataka kukufahamisha kuhusu ‘Building a better tomorrow’ project Mradi huu uliopo hatua za mwanzo sisi wizara tutatenga fedha, kima cha chini 5B kwa kuanzia.

Kwasababu: Vijana hawaendi shambani na hawana motisha kuingia katika kilimo, changamoto za;
1) Upatikanaji wa Mtaji fedha
2) Upatikanaji wa Ardhi
3) Teknolojia
4) Masoko ya uhakika

Manbo haya yote huwakwamisha vijana na watanzania wengi wenye ndoto za kufanya kilimo Kikubwa na chenye tija.

Kwahivyo tumeamua kutengeneza maeneo Maalum ya kilimo (agricultural parks), maeneo haya yatafanyiwa vipimo (soil analysis etc) na upembuzi. Pia tutapeleka miundombinu ya maji na barabara. Baada ya kuweka vyote tutakata vipande shamba (block farms) ambazo tutawakabidhi vijana ambao watapatikana kwa programu maalumu yenye vigezo vya kukidhi.

Rai yangu kwa wadau wa maendeleo tutawafuata kuwaomba fedha tuchange pamoja.

Na lengo letu la msingi ni kuwapatia vijana mitaji hai na yenye tija. Kuanzia kwenye ardhi ambako tutaweka mifumo imara ya umwangiliaji, kuwafunda ukulima bora, tutawasaidia mbegu bora na mbolea ili wazalishe.

Hata hivyo tutawaunganisha vijana hawa na masoko kwajili ya mazao yao.

Jambo la msingi kwakua nia yetu na jambo hili lina tija kubwa hivyo Ardhi na fedha zote tutazitenga, na tutahakikisha tunawasaidia vijana hawa kutumia teknolojia za kisasa na mashine za kisasa za kilimo huku maeneo yote yakiunganishwa na mifumo rasmi ya wanunuzi (Offtakers).

Kwa kuwa na kilimo cha kisasa katika nchinyetu tutaongeza sio tu uzalishaji na ubora wa mazao yetu ili tutapunguza tatizo la ajira, tutahamasisha ushiriki wa vijana wengi kwenye kilimo na kujenga Uchumi endelevu wa nchi yetu."
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe

View attachment 2105306
Hongera sana Mh Bashe uko vizuri
 
Back
Top Bottom