WAZIRI BASHE: Tunaanzisha vituo vya huduma ya pamoja

WAZIRI BASHE: Tunaanzisha vituo vya huduma ya pamoja

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
"Tunaanzisha vituo vya huduma ya pamoja katika maeneo ya Nyanda za juu kusini, katika mpaka wa Namanga pamoja na Dar es Salaam. Uanzishwaji wa vituo hivi unalenga vituo hivi unalenga katika kuongeza thamani ya bidhaa zetu za Tanzania na kuzipa hadhi katika masoko ya kimataifa ikiwa ni pamoja na kutambulisha mahala zinakotoka bidhaa zetu.”

Vituo hivi vitakua na uwezo wa kutoa huduma za ukaguzi, kupanga, Kufungasha na kuhifadhi huku bidhaa zote za kilimo zikiwa na chapa halali ya “Imezalishwa nchini Tanzania”


Hussein Mohammed Bashe
Waziri wa Kilimo

IMG-20220131-WA0101.jpg
 
Hatua nzuri,itakuaje kwa machungwa yanayopakiwa kwenye fuso?
 
Hii nchi sitashangaa ukiambiwa gharama ya kulipia hayo mambo ukajiuliza kwanini nishukue tu marker pen na kuandika Imezalishwa Tanzania

Alafu sababu hawajafanyia market ya kutosha hizo products zao huenda imezalishwa Tanzania ikawa ni disadvantage...

Kwa kuwasaidia wadau aongee na wizara ya biashara n.k. kusaidia hawa watu kupata masoko...., na hilo lingefanyika jana sio leo wala kesho
 
Hatua nzuri,itakuaje kwa machungwa yanayopakiwa kwenye fuso?
utasaidiwa kwenye ukaguzi, kupanga, Kufungasha na kuhifadhi; ila sidhani kama hili litakuwa ni ombi au msaada (as in free)
 
Nakukubali sana. Daaah! Usomali tu ila unafaa kuiongoza TZ
 
Back
Top Bottom