Lituye
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 1,864
- 5,695
Kwanza nianze kusema nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa Mh.Bashe alitamka maneno yale kwa lengo la ubaguzi wa kidini na pia naamini hakutamka kimakosa.
Na pia naamini kuwa Mh. Bashe hawezi kujua kuwa wakristo wapo ktk mfungo kwa kuwa sio tamaduni zao kutangaza wafungapo.
Wakristo wanafunga nyakati nyingi tuu tena kwa walio na imani sukari sio kipaumbele Chao kwa kuwa hata chumvi tuu na uji au maji ya moto yanatosha kwa aliye funga kwa imani na ndio maana pamoja na uhaba wa sukari huwezi sikia mkristo akilalama kwa kuwa kufunga sio starehe kwa wakristo.
Siamini pia utatuzi wa uhaba wa sukari unalengo la kuwanufaisha waislamu. Waislamu wanamatatizo mengi kama raia wengine tunaishi wote huku mtaani. Wapo wanao kufa kwa kukosa huduma bora za kimatibabu au fedha je hao mfungo ni muhimu kwao kuliko uhai wao wakati huu?
Wakati huu vyakula vimepanda bei na mfungo ukianza tuu bei hupanda zaidi, huku uhaba wa umeme, maji, ajira nk. Je matatizo haya Waislamu hayawahusu wakati wa mfungo? Au yatatatuliwa mfungo gani?
Mh.Bashe alipokuwa anasema kuhusu lini tatizo la sukari litaisha awali alieleza vizuri kuwa katikati ya mwezi wa tatu hakuweka neno mfungo. Neno mfungo ameliweka baada ya kurudia kuonesha msisitizo ndio maana nasema hakulisema kimakosa alikusudia.
Kwa sisi tulio somea maana za maana yaani [ Themantics] kule Cuba tunapata maana kuwa lengo la kauli ile ni kujipatia uungwaji mkono miongoni mwa makundi ya kijamii yaani cheap popularity] kuonesha kuwa upo karibu nao na unajali mambo ya maisha yao.
Nikiongea kwa mifano ni kuwa Magufuli aliwahi changisha kanisani michango ili kujenga Msikiti Dodoma. Angefanya hivi muislamu ingekuwa ni habari kubwa kwa katiba gani Rais anahusika na ujenzi wa misikiti na makanisa?
Kwa bahati mbaya kauli ya Bashe imekuja wakati mbaya. Hata kama angesema tatizo litaisha kabla ya sherehe za Pasaka wenye akili bado tungesema ni unafiki tuu na kutaka cheap popularity kwani Pasaka inamuhusu nini yeye.
Maendeleo hayana vyamaa