Waziri Bashungwa akabidhi magari matatu ya Zimamoto yaliyotengenezwa Tanzania, asema "Inawezekana majirani waje kununua magari Tanzania"

Watengeneze mavieite ili waokoe Bilion 500 kwa mwaka.

Leo asubuhi nimeziona v8 latest model zina plate number za JW zimetoka Toyota pale Pugu road
 
Scania iliwahi kuwa na kiwanda cha kuunganisha magari yake pale Kibaha. Iweje sasa Tanzania itengeneze gari la zimamoto liitwalo Nyumbu lakini nembo ya Scania?

Hivi waandishi wa habari huwa mnachapisha kila kitu bila hata kuchunguza?.... 😯 Huu si ndio ukanjanja tena hadharani🤔
 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa amekabidhi magari matatu ya Zimamoto (Mitambo) kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambayo yenye uwezo wa kubeba maji lita 5,000 na Foam Lita 500 kwa kila gari.

Waziri Bashungwa amekabidhi magari hayo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, Alhamisi ya Machi 30, 2023 baada ya kutengenezwa na Shirika la Nyumbu lililopo Kibaha Mkoani Pwani.

Ikielezwa kuwa shirika hilo lililopo chini ya Jeshi la Wananchi limekamilisha matengenezo ya magari hayo na yapo tayari kuanza kazi.

View attachment 2571249

Hafla hiyo ya Makabidhiano imehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Mmuya, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John Masunga, Meneja Mkuu wa Shirika hilo Brigedia Jenerali Hashim Komba, Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Maafisa na Askari kutoka Jeshi la Wananchi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Waziri Bashungwa amesema “Tutaendelea kushirikiana na Wizara nyingine kuhakikisha tunatimiza majukumu yetu, Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza kushirikiana na vyombo vingine kuhakikisha tunaboresha sekta ya viwanda vya ulinzi.

"Pia mchakato huu umeweza kuokoa fedha nyingi ambapo kama mchakato ungefanyika kuagiza magari haya kutoka nje basi gharama yake ingekuwa kubwa zaidi ya iliyotumika.

“Katika Awamu ya Sita kuna fursa ya uwekezaji katika sekta ya ulinzi, kazi iliyofanyika ni ya kiwango cha juu, ndio maana hata walivyokuja Scania ambao tunatumia nembo yao, walishangaa ubora ambao umetumika kutengeneza vichwa vya magari haya ya Zimamoto.

“Scania walisema kwa ubora huu hawaoni kwa nini Tanzania waendelee kuagiza magari ya Zimamoto wakati wana uwezo wa kutengeneza kwa viwango vya kimataifa na kupitiliza.

“Tunajua katika uvumbuzi wa masuala haya kuna fursa ya kufanya maboresho, inawezekana kuna changamoto zimetokea wakati wa mchakato, hivyo pale ambapo kuna fursa ya kufanya vizuri zaidi, kaeni mezani muangalie wapi kwenye mapungufu ili muone mnavyoweza kuboresha.

“Mnaweza kutengeneza magari kwa ajili ya vyombo vyetu lakini pia si ndoto kwamba mnaweza kutengeneza hata kwa majirani zetu, sioni kama ni ndoto hilo kutokea kwa Nchi za jirani kuja Tanzania kununua magari hapa TATC Nyumbu.”

Naye, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akizungumza katika hafla hiyo amesema:

“Wakati fulani ilipotokea kuna tukio la uzimaji moto, Jeshi la Zimamoto lilikuwa linakwenda kufedhehesha badala ya kusaidia, lakini kuimarisha nyenzo, ajira, uwezo, mafunzo na vifaa, kutawawezesha kufanya kazi kwa ufanisi wa juu wakati wa majanga.

“Kinachofanyika ni mwendelezo wa jitihada za Awamu ya 6 katika kuwezesha maboresho ya vyombo vya ulinzi na usalama.

“Napongeza kazi kubwa ya TATC Nyumbu ambao wametoa miaka miwili kwa magari haya yanayokabidhiwa yatakuwa yanafanyiwa ‘service’, natoa wito wahusika msiruke matengenezo pale inapotakiwa.”

Upande wa Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali Masunga amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kuahidi kuyatunza magari hayo na kuendelea kuwahudumia wananchi katika huduma za Kuzima Moto na Uokoaji.
Hizo ni scania acheni uongo na upotoshashaji
 
Khna watu sjui ni vizazi vya ngapi humu,Moshi kuna kiwanda cha cocacola,Mwanza kuna kiwanda cha Pepsi,hii inawezekanaje?
 
Ninyi wenyewe hamjajitishea mnataka wanunuzi.
Mambo gani hii.
Hizi 3 zenyewe utakuta ni nguvu kubwa na presha kutoka juu ndio zikakamilika,halafu wanataka waanze kuuza,usanii tu
 
CAG kataja haya magari kwenye ripoti yake
 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa amekabidhi magari matatu ya Zimamoto (Mitambo) kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambayo yenye uwezo wa kubeba maji lita 5,000 na Foam Lita 500 kwa kila gari.

Waziri Bashungwa amekabidhi magari hayo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, Alhamisi ya Machi 30, 2023 baada ya kutengenezwa na Shirika la Nyumbu lililopo Kibaha Mkoani Pwani.

Ikielezwa kuwa shirika hilo lililopo chini ya Jeshi la Wananchi limekamilisha matengenezo ya magari hayo na yapo tayari kuanza kazi.

View attachment 2571249

Hafla hiyo ya Makabidhiano imehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Mmuya, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John Masunga, Meneja Mkuu wa Shirika hilo Brigedia Jenerali Hashim Komba, Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Maafisa na Askari kutoka Jeshi la Wananchi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Waziri Bashungwa amesema “Tutaendelea kushirikiana na Wizara nyingine kuhakikisha tunatimiza majukumu yetu, Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza kushirikiana na vyombo vingine kuhakikisha tunaboresha sekta ya viwanda vya ulinzi.

"Pia mchakato huu umeweza kuokoa fedha nyingi ambapo kama mchakato ungefanyika kuagiza magari haya kutoka nje basi gharama yake ingekuwa kubwa zaidi ya iliyotumika.

“Katika Awamu ya Sita kuna fursa ya uwekezaji katika sekta ya ulinzi, kazi iliyofanyika ni ya kiwango cha juu, ndio maana hata walivyokuja Scania ambao tunatumia nembo yao, walishangaa ubora ambao umetumika kutengeneza vichwa vya magari haya ya Zimamoto.

“Scania walisema kwa ubora huu hawaoni kwa nini Tanzania waendelee kuagiza magari ya Zimamoto wakati wana uwezo wa kutengeneza kwa viwango vya kimataifa na kupitiliza.

“Tunajua katika uvumbuzi wa masuala haya kuna fursa ya kufanya maboresho, inawezekana kuna changamoto zimetokea wakati wa mchakato, hivyo pale ambapo kuna fursa ya kufanya vizuri zaidi, kaeni mezani muangalie wapi kwenye mapungufu ili muone mnavyoweza kuboresha.

“Mnaweza kutengeneza magari kwa ajili ya vyombo vyetu lakini pia si ndoto kwamba mnaweza kutengeneza hata kwa majirani zetu, sioni kama ni ndoto hilo kutokea kwa Nchi za jirani kuja Tanzania kununua magari hapa TATC Nyumbu.”

Naye, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akizungumza katika hafla hiyo amesema:

“Wakati fulani ilipotokea kuna tukio la uzimaji moto, Jeshi la Zimamoto lilikuwa linakwenda kufedhehesha badala ya kusaidia, lakini kuimarisha nyenzo, ajira, uwezo, mafunzo na vifaa, kutawawezesha kufanya kazi kwa ufanisi wa juu wakati wa majanga.

“Kinachofanyika ni mwendelezo wa jitihada za Awamu ya 6 katika kuwezesha maboresho ya vyombo vya ulinzi na usalama.

“Napongeza kazi kubwa ya TATC Nyumbu ambao wametoa miaka miwili kwa magari haya yanayokabidhiwa yatakuwa yanafanyiwa ‘service’, natoa wito wahusika msiruke matengenezo pale inapotakiwa.”

Upande wa Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali Masunga amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kuahidi kuyatunza magari hayo na kuendelea kuwahudumia wananchi katika huduma za Kuzima Moto na Uokoaji.
Mbona kichwa kimeandikwa SCANIA badala ya NYUMBU?🙄🙄🙄
 
Tofautisha kutengeneza na kuunganisha ....hiyo unasoma kabisa ni scania kwa hiyo hawajatengeneza bali wameunganisha tu parts
 
Back
Top Bottom