Waziri Bashungwa jiuzulu kuepuka laana inayomnyemelea Dkt. Hassan Abbas

KooZito

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2020
Posts
397
Reaction score
1,377
Tahadhima kwenu wanabodi

Naomba kutumia sikukuu hii ya Mapinduzi kumpa ushauri usiolipiwa kwa kijana Waziri wa Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni, Innocent Lugha Bashungwa kama anataka kuendelea kubaki kwenye ulingo wa siasa za Tanzania.

Wizara uliyopewa ni nyeti na "ngumu kumeza". Ni wizara ambayo kwa unyambuzi ilistahili iwe na wizara zaidi ya tatu. Hapo kuna Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Ushauri wangu kwako Bashungwa ni katika sekta ya Habari.

Shabaha ya kukushauri Bashungwa ni kukufanya ubaki kuwa "Innocent" kama jina lako. Uepuke hatia na laana zinazomtafuna Katibu wako Dkt. Hassan Abbas ambaye mbali na kuwa Msemaji wa Serikali pia ndiye bosi wa Waandishi wa Habari pale Idara ya Habari, MAELEZO.

Kama kuna sekta iliyoathirika katika utawala wa Rais Magufuli ni Habari. Hakuna ubishi kuwa Magufuli si rafiki hata kidogo na vyombo vya habari na hata wanahabari. Waandishi wa Habari makini wanaojua kazi yao wataendelea kuwa maadui wa utawala wa Rais Magufuli. Baadhi yetu wanaamini kuwa ni mtu mwoga wa kukosolewa hata kama ni kwa nia njema ya kujenga nchi.

Historia imebaki kuwa katika utawala huu vyombo vingi sana vya habari hususan magazeti yamefungiwa. Waandishi wamefungwa, wametishwa, wamefunguliwa mashitaka, wameteswa, wamedhihakiwa. Baadhi yao hasa nguli wa tasnia wamesalimu amri na kuweka kalamu chini.

Bashungwa, imepewa wizara ambayo imesimamia na kuratibu kudhibiti Uhuru wa Habari tena kwa kutunga Sheria kandamizi na katili. Baada ya JPM kuingia madarakani tumeona Sheria ya mitandao ya kijamii ikivifuta "blogs" nyingi sana hewani.

Serikali ikajisahaulisha kuwa chombo cha habari ni kampuni sawa na kiwanda. Kina wafanyakazi na waajiriwa wengi. Unapokifunga kiwanda au kampuni unaondoa dhana nzima ya uchumi wa viwanda. Lakini kwa utawala huu waandishi wa Habari hawaonekani kama wafanyakazi. Baada ya kufunga vyombo vingi vya habari ushahidi upo wa wanahabari wengi sasa wamebaki malofa na "matonya" mitaani kana kwamba ni taaluma isiyohitajika. Waandishi wengi wanatia huruma mitaani. Hivi, kama mtu kasomea udaktari au uhasibu unamfukuza kazi akafanye kazi ya taaluma gani ambayo hakusomea? Kwa nini waandishi wanakatiliwa namna hii? Kwa nini ni rahisi kumwambia mwandishi akafanye kazi nyingine lakini haiwi hivyo kwa madaktari?

Wizara yako hii pia ina mchafukoge. Kuna mwingiliano wa kiutendaji kwa wanahabari. Mfano, TCRA iko chini ya wizara ya Mawasiliano na Teknolojia. Lakini wahudumu wa Televisheni na Redio ni Waandishi wa Habari wale wale wanaopewa Press Card na MAELEZO iliyo chini ya wizara nyingine. Hapa kuna tatizo.

Bashungwa umenukuliwa ukisema wizara yako inafikiria uamuzi wa TCRA kukifungia Wasafi Tv ukizingatia ajira zao nk na kwamba wameomba msamaha. Hebu angalia mafaili mezani kwako kupitia kwa Dk. Abbas ni vyombo vingapi vya habari viliomba radhi lakini vimefungiwa kwa muda usiojulikana? Kwani huko hakuna ajira? Orodha yao ni ndefu sana!

Mhe Innocent, kama kweli unataka kutenda haki na kusimamia haki, kutenda kwa kujiamini pasipokuogopa mteuzi wako kukufurusha ofisini, basi pitia maamuzi yote ya hovyo yaliyofanywa na Nape Nnauye, Dk. Mwakyembe chini ya usimamizi wa Dk. Abbas ambaye jopo la Wahariri na Waandishi wakongwe sasa wanamtafutia dawa ikiwa ni pamoja na kumzomea hadharani akikutana nao muda wowote kwa kuunga mkono unyanyasaji wa Waandishi habari nchini.

Hii inakufanya Bashungwa kuchagua njia moja kati ya mbili: kuungana na Dk. Abbas kutesa tasnia ya Habari au kufumua uhovyo wote ulioasisiwa na Nape na Dk. Abbas potelea mbali kama utafukuzwa kazi lakini tasnia ya Habari na wanahabari "watakuajiri" na kukukumbuka kwa kuwakumbuka.

Wanahabari wanasikitishwa na hatua ya Dk. Abbas kitaaluma kuona "the so called" magazeti yanayomwimbia nyimbo za sifa JPM hata kwa mambo ya hovyo ndiyo ya maana na serious papers ndio adui. Chanja za magazeti kwa sasa ni aibu kwa habari na mwenyewe unajionea.

Wewe bado ni kijana katika siasa. Hujachafuka kwa uwazi. Usiogope kufukuzwa kazi kutetea sekta ya habari na Uhuru wa habari. Acha alama nyuma yako. Ni waandishi hawa hawa watakaokubeba.

Mwisho ni wito kwa wanahabari. Unganeni. Umoja wenu ndio nguvu yenu. Hakuna duniani mtawala aliyeshindana na media akashinda. Anaweza kuhisi ushindi kwa muda tu lakini mwisho wa siku ni aibu na fedheha kama Al-Bashir. Mlioacha kalamu zichukueni kwa mara nyingine maana ndio silaha yenu. Maiogope wanaotesa na kuua mwili, ogopeni anayeua roho zenu. Msiache kupambana.

Mapinduziii......

Nawasilisha kwa heshima.
 
Basically, every cadre has been impaired. Not only news writers,think of doctors, nurses, teachers, etc. Are all these reasonably employed.
 
Hiyo Wasafi ni ya mtu wao huwa anawafaa wakati wa kampeni, lazima wamfikirie, najiuliza kama Tanzania Daima nao wangeomba msamaha sidhani hata kama wangesikilizwa.
 
Nimecheka kwa nguvu, Paskali Mayalla huwa anasema wapinzani hawana mwelekeo na kuwa eti ccm ya sasa ni imara! Muulize lini aliwahi kukaa na kiongozi yoyote wa serikali kisha akamuuliza maswali magumu, na kupata majibu kama zamani? Kuna mwenzake anaitwa Manyerere Jackton, wamegeuka mitume wa Magu, wanaongea vitu vya ajabu mpaka ni aibu.
 
Hii niaina nyingine ya ujinga wa Mtanzania.

Unajua kabisa watanzania hatuna utamaduni wa kukiuzuri. Leo Unatoka na pwndekezo hilo.

Wewe toa njia kutatua hizo changamoto.

Mtu Anamda mfupi tu kazini ajiuzuru?

Hii ni sawa na kusema kila anae teuliwa akatae.
 
Wabongo wanafiki Sana, hebu jiulize katika Hali halisi Kama ungekuwa wewe ungeachia uwaziri kwa sababu ulizozitaja?

Haishangazi hata wewe ukiteuliwa ndiyo utakuwa katili kupita kiasi.

#Mit5no Teana!
Hata hakuchukua muda kuwakumbuka "waliookotwa JALALANI" wakati anaandika aliyoyaweka hapa!

Lakini hata hao aliowataja hapo, akina Nape na Mwakyembe, na wengi wengine waliobadilika baada ya upepo wa "asiyepangiwa" ulipowavumia.

Huyo Abbas kawekwa hapo kwa sababu ameonyesha ndiye anayeiweza kazi ya kuwanyamazisha wote.

Huyo kijana Bashungwa hana ubavu wa kufanya lolote mleta mada anayomshauri. Hapo aondoe mategemeo kabisa. Kwanza kijana wa watu hana 'track' record yoyote inayoonyesha kwamba anaweza kufanya maamuzi yasiyomtegemea mteuzi wake, sasa sijui huo ujasiri atautoa wapi?
Ktk dunia ya leo hamna chombo chenye nguvu kuzidi media ..afu chakushangaza mnakua goigoi..
Sijui waanzie wapi mkuu 'Querido'. Si unaona hao wanaonyanyua pua zinakatwa na vyombo vyao kufungiwa. Sasa sijui wewe unapendekezo wafanye nini?
Mwisho ni wito kwa wanahabari. Unganeni. Umoja wenu ndio nguvu yenu. Hakuna duniani mtawala aliyeshindana na media akashinda. Anaweza kuhisi ushindi kwa muda tu lakini mwisho wa siku ni aibu na fedheha kama Al-Bashir. Mlioacha kalamu zichukueni kwa mara nyingine maana ndio silaha yenu. Maiogope wanaotesa na kuua mwili, ogopeni anayeua roho zenu. Msiache kupambana.
Pole sana.
Lakini kwa sasa, na hasa hapa, mtawala hana mshindani, kwani kadhibiti vilivyo hadi kukosesha sehemu ya kupumulia. Hao unaowaambia wataanzia wapi kama hata hiyo kazi waliyosomea hawana nyenzo tena za kuifanya?
Washauri wafanye nini ili wajikomboe. Haya uliyoandika kwenye mada hii, pamoja na kwamba yanatia masikitiko makubwa, lakini haisaidii kitu chochote bila kushauri nini hasa kifanyike ili uhuru wao wa kufanya kazi walizozisomea urejeshwe tena.

Bashungwa, mwache afaidi ajira aliyopewa. Hana uwezo wowote wa kubadili lolote ndani ya wizara hiyo. Huyo kajaza tu nafasi hiyo isionekane haina mtu. Yeye ni ki'robot' tu kilichowekwa kutumika hapo.
 
Nimecheka kwa nguvu, Paskali Mayalla huwa anasema wapinzani hawana mwelekeo na kuwa eti ccm ya sasa ni imara! Muulize lini aliwahi kukaa na kiongozi yoyote wa serikali kisha akamuuliza maswali magumu, na kupata majibu kama zamani? Kuna mwenzake anaitwa Manyerere Jackton, wamegeuka mitume wa Magu, wanaongea vitu vya ajabu mpaka ni aibu.
Hivi huyo uliyemtaja hapo (wa kwanza) kishapata uteuzi popote?

Kateuliwa kimya kimya kufanya kazi maalum, ambayo ndiyo huenda inamfanya asionekane huku akijaza magazeti (makala zake ndefu zisizo na mwelekeo) humu?
 
Huyo wakwanza amekata tamaa,povu la mapambio limeisha.
 
Tahadhima kwenu wanabodi

Naomba kutumia sikukuu hii ya Mapinduzi kumpa ushauri usiolipiwa kwa kijana Waziri wa Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni, Innocent Lugha Bashungwa kama anataka kuendelea kubaki kwenye ulingo wa siasa za Tanzania.

Wizara uliyopewa ni nyeti na "ngumu kumeza". Ni wizara ambayo kwa unyambuzi ilistahili iwe na wizara zaidi ya tatu. Hapo kuna Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Ushauri wangu kwako Bashungwa ni katika sekta ya Habari.

Shabaha ya kukushauri Bashungwa ni kukufanya ubaki kuwa "Innocent" kama jina lako. Uepuke hatia na laana zinazomtafuna Katibu wako Dkt. Hassan Abbas ambaye mbali na kuwa Msemaji wa Serikali pia ndiye bosi wa Waandishi wa Habari pale Idara ya Habari, MAELEZO.

Kama kuna sekta iliyoathirika katika utawala wa Rais Magufuli ni Habari. Hakuna ubishi kuwa Magufuli si rafiki hata kidogo na vyombo vya habari na hata wanahabari. Waandishi wa Habari makini wanaojua kazi yao wataendelea kuwa maadui wa utawala wa Rais Magufuli. Baadhi yetu wanaamini kuwa ni mtu mwoga wa kukosolewa hata kama ni kwa nia njema ya kujenga nchi.

Historia imebaki kuwa katika utawala huu vyombo vingi sana vya habari hususan magazeti yamefungiwa. Waandishi wamefungwa, wametishwa, wamefunguliwa mashitaka, wameteswa, wamedhihakiwa. Baadhi yao hasa nguli wa tasnia wamesalimu amri na kuweka kalamu chini.

Bashungwa, imepewa wizara ambayo imesimamia na kuratibu kudhibiti Uhuru wa Habari tena kwa kutunga Sheria kandamizi na katili. Baada ya JPM kuingia madarakani tumeona Sheria ya mitandao ya kijamii ikivifuta "blogs" nyingi sana hewani.

Serikali ikajisahaulisha kuwa chombo cha habari ni kampuni sawa na kiwanda. Kina wafanyakazi na waajiriwa wengi. Unapokifunga kiwanda au kampuni unaondoa dhana nzima ya uchumi wa viwanda. Lakini kwa utawala huu waandishi wa Habari hawaonekani kama wafanyakazi. Baada ya kufunga vyombo vingi vya habari ushahidi upo wa wanahabari wengi sasa wamebaki malofa na "matonya" mitaani kana kwamba ni taaluma isiyohitajika. Waandishi wengi wanatia huruma mitaani. Hivi, kama mtu kasomea udaktari au uhasibu unamfukuza kazi akafanye kazi ya taaluma gani ambayo hakusomea? Kwa nini waandishi wanakatiliwa namna hii? Kwa nini ni rahisi kumwambia mwandishi akafanye kazi nyingine lakini haiwi hivyo kwa madaktari?

Wizara yako hii pia ina mchafukoge. Kuna mwingiliano wa kiutendaji kwa wanahabari. Mfano, TCRA iko chini ya wizara ya Mawasiliano na Teknolojia. Lakini wahudumu wa Televisheni na Redio ni Waandishi wa Habari wale wale wanaopewa Press Card na MAELEZO iliyo chini ya wizara nyingine. Hapa kuna tatizo.

Bashungwa umenukuliwa ukisema wizara yako inafikiria uamuzi wa TCRA kukifungia Wasafi Tv ukizingatia ajira zao nk na kwamba wameomba msamaha. Hebu angalia mafaili mezani kwako kupitia kwa Dk. Abbas ni vyombo vingapi vya habari viliomba radhi lakini vimefungiwa kwa muda usiojulikana? Kwani huko hakuna ajira? Orodha yao ni ndefu sana!

Mhe Innocent, kama kweli unataka kutenda haki na kusimamia haki, kutenda kwa kujiamini pasipokuogopa mteuzi wako kukufurusha ofisini, basi pitia maamuzi yote ya hovyo yaliyofanywa na Nape Nnauye, Dk. Mwakyembe chini ya usimamizi wa Dk. Abbas ambaye jopo la Wahariri na Waandishi wakongwe sasa wanamtafutia dawa ikiwa ni pamoja na kumzomea hadharani akikutana nao muda wowote kwa kuunga mkono unyanyasaji wa Waandishi habari nchini.

Hii inakufanya Bashungwa kuchagua njia moja kati ya mbili: kuungana na Dk. Abbas kutesa tasnia ya Habari au kufumua uhovyo wote ulioasisiwa na Nape na Dk. Abbas potelea mbali kama utafukuzwa kazi lakini tasnia ya Habari na wanahabari "watakuajiri" na kukukumbuka kwa kuwakumbuka.

Wanahabari wanasikitishwa na hatua ya Dk. Abbas kitaaluma kuona "the so called" magazeti yanayomwimbia nyimbo za sifa JPM hata kwa mambo ya hovyo ndiyo ya maana na serious papers ndio adui. Chanja za magazeti kwa sasa ni aibu kwa habari na mwenyewe unajionea.

Wewe bado ni kijana katika siasa. Hujachafuka kwa uwazi. Usiogope kufukuzwa kazi kutetea sekta ya habari na Uhuru wa habari. Acha alama nyuma yako. Ni waandishi hawa hawa watakaokubeba.

Mwisho ni wito kwa wanahabari. Unganeni. Umoja wenu ndio nguvu yenu. Hakuna duniani mtawala aliyeshindana na media akashinda. Anaweza kuhisi ushindi kwa muda tu lakini mwisho wa siku ni aibu na fedheha kama Al-Bashir. Mlioacha kalamu zichukueni kwa mara nyingine maana ndio silaha yenu. Maiogope wanaotesa na kuua mwili, ogopeni anayeua roho zenu. Msiache kupambana.

Mapinduziii......

Nawasilisha kwa heshima.
Ikiwa mtoa mada ni mojawapo wa wahahabari nampapongezi zake ,kwani leo hii pamoja na madhila yote kwa wanahabari na watanzania waimba mapambio no 1 ni wanahabari wenyewe hata uovu utasifiwa.
 
Hata Rais wa Marekani Bw. Trump amefungiwa kwenye socia media zote!! Sasa sijui nao huko maulaya wana laana???
 
Back
Top Bottom