Eric Cartman
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 11,966
- 11,218
Kuelewa kinachoendelea ni jukumu la EWURA, wizara kutoa maelezo au vyombo vya habari; ni kwa sababu hakuna communication kutoka kwa hao wahusika inabidi wananchi wenyewe tuanze kujiuliza na kujazia majibu kama tunavyofanya kwenye hii mada (the conclusion might not be certain).Hili somo ndilo tunatakiwa tupewe, kwanza tulishazoea mafutab ya 2200 hawa wakapunguza mpaka 1500 tukiwa 2200 haya matatizo hayakuwepo basis bora turudi kama zamani lakini tuyapate, mafuta hatuchimbi wenyewe hatuwezi jipangia huo ndio ukweli. Lakini mbona kituo cha boko magengeni hayajawahi kuisha? Wanayapata wapo?
Soma post number #61 utaona kwenye hiyo habari tatizo la refineries za US kwenye post #52 ndio hilo hilo la Asians refiniries na most chances huko ndio tunapoagiza mafuta.
Refiners wote wanadai kutokana na low demand ya mafuta duniani imebidi Saudi Arabia washushe bei wao wenyewe ya Crude Oil (without market forces) kuwasaidia refiniries ili wapunguze hasara, maana yake nini low demand + plus fixed costs za kusafisha mafuta; refiniries ata wasiposhusha bei pamoja na kwamba wananunua rahisi bado wanatengeneza hasara au margin zao ni ndogo sana.
Ndio maana wameomba Saudi Arabia washushe bei walau waweze pata faida aina maana wao kushushiwa bei na wao watapunguza kwa suppliers maana awauzi sana kwa ivyo logic ni kwamba itawasaidia kupunguza production costs tu kwa sasa.
Ndio maana kunasababu ya kufanya uchunguzi badala ya kusikiliza malalamiko ya upande mmoja.
Hiko kituo cha mafuta cha Boko siwezi elewa labda kina reserve kubwa ya tank, volumes za watumiaji sio sana or whatever the case hilo swala atakuwa analijua manager wa kituo; I am only speaking generally.