Waziri Biteko asema Tanzania ipo tayari kwa kongamano kubwa la Madini, aelezea kinachokwamisha biashara ya Chumvi

Waziri Biteko asema Tanzania ipo tayari kwa kongamano kubwa la Madini, aelezea kinachokwamisha biashara ya Chumvi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kuelekea Kongamano la Uwekezaji katika Sekta ya Madini Mwaka 2023 linalojulikana kwa jina la Tanzania Mining & Investment Forum 2023, Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema wamepanga kutoa elimu kubwa zaidi kuelekea shughuli hiyo itakayofanyika baadaye mwaka huu ili sekta ya Madini ikue Nchini.

Amesema Wizara ya Madini kila Februari ya kila Mwaka inafanya mkutano wa Mwaka, safari hii kutokana na wingi wa mikutano ya kimataifa katika mataifa mengine imebidi wabadilishe ratiba ambapo safari hii utafanyika Oktoba 25-26, 2023.

Amesema “Mwaka huu tutakuwa na wazungumzaji wengi, Wadau kutoka Serikalini, Mawaziri, wataalamu mbalimbali, makampuni ya madini, lengo ni kuwapa watu maisha bora na jinsi ya kukuza sekta ya madini.

“Tanzania ipo tayari kwa mkutano huo na ndio maana kumekuwa na mikutano midogomidogo mingi kuelekea mkutano huo mkubwa.”

Ameongeza kuwa “Awali, kundi moja la madini fulani lilikuwa na uwezo wa kutawala mkutanoni kutokana na wingi wao na kuwafanya wengine kutokuwa na sauti, hali hiyo imesababisha hasara kwa kuwa kundi moja linameza makundi mengine kiasi yanashindwa kutoa michango yao.

“Tutaendelea kukutana na Wadau wa madini kwa kuwa mkutano huo utakuwa wa kipekee, tutaunganisha sekta ya madini na utalii.”

Anasema “Uchimbaji Majini umegawanyika katika makundi matatu ambayo ni uchimbaji mkubwa zaidi ya Dola 100, uchimbaji wa kati Dola Milioni 10-99 na wachimbaji wadogo ambao ni 0 hadi Dola Milioni 9.

“Huko nyuma wachimbaji wa dogo mchango wao ulikuwa hawonekani, lakini baada ya mabadiliko ya Sheria na kuwapatia nafasi nao wamechangamkia fursa na ndio maana mauzo ya mwaka uliopita mchango wao umetoka 4% hadi 40%.”

Akitolea Mji wa Kahama na Geita unaendeleza kwa asilimia kubwa na Wachimbaji wadogo, kwa kuwa wameachana na mfumo wa zamani kuwa wakipata fedha wanazitumia hadi ziishe kisha wanarudi tena kuchimba, kwa sasa wanawekeza na wanapata maendeleo.

Afafanua Tanzania ilivyo na utajiri wa Chumvi
Kuhusu Biashara ya Chumvi Nchini amesema “Nataka niwaambie Watanzania wenzangu tunatakiwa kubadili fikra zetu, tutumie chumvi tunayozalisha wenyewe.

“Tuna Pwani ndefu kuliko majirani zetu, ni aibu kubwa una Pwani ya zaidi ya Kilometa 500 kisha unatumia chumvi ya mtu mwenye Pwani ya Kilometa 200, wao wametumia soko lao kuzalisha chumvi na soko lao linakuja kwetu.

"Tutakapoanza kuifanya chumvi kama biashara ndio tutaona umuhimu wake, kwa kuwa pia tutaajiri watu wengi, mfano Mtwara na Lindi biashara ya chumvi ni nyingi lakini chumvi nyingi tunapata kutoka nje ya nchi.

“Inatakiwa ifike hatua watu wetu watengeneze chumvi kwa ubora ili wauze kwa watu wetu, mambo mengine ya kusingiziana na vita vya kibiashara ili watu wasizalishe wengine waendelee kuleta chumvi za nje.”
3-47.jpg

Waziri wa madini nchini Dkt. Doto Biteko akimsikiliza Mkurugenzi wa Ocean Business Patners Tanzania Ltd Abdulsamad Abdulrahim wakati akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali
6-18.jpg
5-29.jpg
4-35.jpg
Picha zikionesha wadaumbalimbali wakishiriki katika mkutano huo uliofanyikakwenye hpteli ya Hyyat Regency jijini Dar es Salaam Mei 23,2023
 
Back
Top Bottom