The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
"Hoja nyingine imekuwa ni upungufu wa wafanyakazi ambayo Waheshimiwa wabunge wameeleza, nataka nitoe tu taarifa kuwa tumepata kibali cha kuajiri watumishi 570 kwa mwaka 2024/25, utaratibu unakamilishwa, watumishi hao waweze kupangiwa majukumu yao.
Serikali pia imepanga kuajiri watumishi wengine 1,000 katika mwaka wa fedha 2025/26 ili kukabiliana na changamoto ya upungufu katika maeneo mengine na Mhe. Spika kadri tunavyoendelea kusambaza umeme ndiyo mahitaji yanavyoongezeka ya watu kuhudumia hizo line, kwahiyo tumepata nafasi ya kuajiri watu wengi zaidi ili tuweze kufanya kazi.
Waheshimiwa wabunge tembeeni kifua mbele mkiamini kuwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamua kuijenga hii nchi tena sio kwa maneno, Mhe. Rais anapenda kusema kidogo na kutenda zaidi. Ametufundisha falsafa ya nia njema huwa haishindwi, Tembeeni mkiwa na nia njema ya kuwahudumia watanzania na mimi ninaamini kwasababu nia njema haishindwi ninyi mtaibuka washindi na Mungu awasaidie."
Waziri Biteko akihitimisha mjadala wa bajeti ya Wizara yake