Angel Msoffe
JF-Expert Member
- Jun 21, 2011
- 6,781
- 1,647
Habari zilizotufikia jioni hii zinasema kwamba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina-Ompeashi-Kombani (pichani), amefariki dunia leo huko India alikokuwa akipata matibabu ya saratani.-
Taarifa kutoka ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na kueleza kwamba mwili wa marehemu unategemewa kuwasili Dar es salaam siku ya Jumatatu, ambapo Bunge na Serikali zitasimamia maandalizi yote ya maziko na kumsafirisha kwa mazishi nyumbani kwa marehemu huko Mahenge ambako alikuwa Mbunge wa jimbo la Ulanga.-
Ni Kweli!!!Alikuwa anaumwa?
Kama ni kweli, poleni wafiwa..
Moses Machali atayakumbuka maneno ya huyu mama milele
Watanzania akili zetu zimeingiliwa na kitu gani lakini? Hapa tumeletewa tanzia ya kifo ya Mtanzania mwenzetu,badala ya kuhungana na kumuombea apumzike kwa amani peponi, sisi tunatanguliza masuala ya itikadi za vyama na kejeli juu, tunajisahau kabisa kuwa kila nafsi itaonja muhuti!! Huku kama sio kuchanganyikiwa ni nini?
Sio huyo mzee hapa kwetu mnyika anapambanana senera mpangara kama sijakosea jina .