TANZIA Waziri Celina Ompeshi Kombani afariki dunia

TANZIA Waziri Celina Ompeshi Kombani afariki dunia

Kama siasa za nchi hii zimefikia hatua ya kuwawafanya wafuasi na baadhi ya wanachama wengine kufurahia na kuthubutu kusema "sijasikitishwa na kifo cha fulani hata hata kidogo" kwa sababu ya uanachama wake basi tumefikia pabaya sana.

Mtu mwenye roho ya namna hii anaweza hata kukuua kwa sumu kwa sababu tu ya tofauti za kiitikadi ya kisiasa.

Kifo kila mmoja atakipitia, uwe CCM, CHADEMA, CUF, ACT and whatever utauonja tu umauti. Na hujui wewe usiyehuzunishwa na kifo cha binadamu mwenzio kifo chako kitakuwaje.

Poleni sana ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu na poleni wanaulanga kwa kuondokewa na mbunge wenu.
 
it is so sad! Why did it happen?
Nasikitika Kuwapa taarifa ya kifo cha Waziri wetu, Celina Kombani kilichotokea huko India..

Celina.jpg


Celina Ompeshi Kombani (19 June 1959 - 24 September 2015) was a Tanzanian CCM politician and Member of Parliament for Ulanga East constituency since 2005.

She was the Minister of State in the President's Office for Public Service Management.
 
Hakuna ajuae saa wala siku ya kufa. Uhakika tuliona ni kuwa siku moja kifo kitatoke
 
Habari zilizotufikia jioni hii zinasema kwamba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina-Ompeashi-Kombani (pichani), amefariki dunia leo huko India alikokuwa akipata matibabu ya saratani.-

Taarifa kutoka ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na kueleza kwamba mwili wa marehemu unategemewa kuwasili Dar es salaam siku ya Jumatatu, ambapo Bunge na Serikali zitasimamia maandalizi yote ya maziko na kumsafirisha kwa mazishi nyumbani kwa marehemu huko Mahenge ambako alikuwa Mbunge wa jimbo la Ulanga.-
 
Tutakukumbuka daima kwa kutusaidia kuipata Wilaya mpya ya Malinyi, wewe ni alama ndani yetu na utaishi ndani ya mioyo ya vizazi vya wana Ulanga,Kilombero na Malinyi. Tangulia shangazi Celina Ompeshi Kombani, wewe hukuwa Vayenda na Wutwa...Ulirudi kutuenzi Vatwa. Amin.
 
Punguza mbwembwe
Kufa kufa tu unafiki wa nn MTU km hana huzuni c bac kwan cku MTU ukifa watu wakilialia au RIP nyingi zinasaidia nn

Duh...

Ni namna tu ya watu kujipa faraja maana ndilo jambo pekee aliye hai hupaswa kufanya...

Ndio utamaduni huo hivyo usipate fukuto la moyo, ajuaye marehemu alipo ni Mungu pekee...
 
Alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa gani? Pumzika kwa amani mheshimiwa.
 
Back
Top Bottom