Waziri Dkt. Doroth Gwajima: Unyanyasaji wa Watoto, 60% unatokea nyumbani

Waziri Dkt. Doroth Gwajima: Unyanyasaji wa Watoto, 60% unatokea nyumbani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Hali ya unyanyasaji wa Watoto Nchini imetajwa kuchangiwa na mmomonyoko wa maadili katika jamii, wengine wakisingizia hali ngumu ya kiuchumi inawafanya kutokuwa na muda wa kulinda na kutoa malezi chanya, ambapo asilimia 60 ya unyanyasaji wa Watoto unatokea nyumbani.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Doroth Gwajima amesema Watoto wanakosa maadili, kwa sababu hawatunzwi vizuri na wazazi.

“Inapotokea kuna mgogoro wa ndoa, wazazi wakitengana bila utaratibu wa kuzingatia malezi ya watoto, matokeo yake Watoto wanakimbilia mtaani,” - Dkt. Gwajima

Source: ITV
 
Malezi yamekuwa changamoto sana sikuhizi, hakuna wa kumwamini ili kuepuka disappointments.
 
Back
Top Bottom