Waziri Dkt. Kijaji Akabidhi Boti za Uvuvi Zenye Thamani ya Bilioni 2

Waziri Dkt. Kijaji Akabidhi Boti za Uvuvi Zenye Thamani ya Bilioni 2

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

WAZIRI DKT. KIJAJI AKABIDHI BOTI ZA UVUVI ZENYE THAMANI YA BILIONI 2​

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amekabidhi boti 13 za Uvuvi zenye thamani ya takribani shilingi Bil. 2 kwa Vikundi vya mikoa ya Pwani na Dar-es-salaam ambazo zinatarajiwa kuwanufaisha zaidi ya Wavuvi 205 wa mikoa hiyo.

Mhe. Dkt. Kijaji amekabidhi boti hizo Julai 16, 2025 kwenye ufukwe wa Shirika la Uvuvi nchini (TAFICO) ambapo mkoa wa Pwani umekabidhiwa Boti 8 huku mkoa wa Dar-es-Salaam ukikabidhiwa boti 5 zote jumla zikiwa na uretu wa mita 12 na 14 ambazo zinajumuisha vifaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Nyavu, kamba, maboya, nyuzi, kitafuta samaki na boti saidizi maarufu kama dingi.

Aidha Mhe. Dkt. Kijaji amebainisha kuwa ugawaji wa boti hizo ni sehemu ya mkakati wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan uliolenga kuboresha sekta ya Uvuvi nchini ambapo wanufaika wanajumuisha makundi manne ambavyo ni watu binafsi, makampuni na vikundi vya Wavuvi.

Boti hizo zilizotolewa leo ni sehemu ya Boti 120 zinazotarajiwa kutolewa kwenye awamu ya pili ya Mkopo huo wenye masharti nafuu ambapo mpaka kukamilika kwa awamu zote mbili jumla ya Boti 280 zinatarajiwa kukopeshwa kwa Wavuvi nchini.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2025-07-16 at 23.17.52.mp4
    20.3 MB
Wakati mkiyafanya hayo mzingatie pia Mikoa kama Lindi na Mtwara yenye bahari ya Hindi pia inakabiliwa na upungufu mkubwa kitoea bora cha Samaki kutokana ma dhana duni za uvuvi wazitumiazo wavuvi wadogo wadogo. IFIKE KIPINDI WATIZAME KWA UMAKINI SWALA HILI PIA.
 
Back
Top Bottom