Waziri Dkt. Ndumbaro Aielekeza Bodi ya Filamu Kushirikiana na Sekta Binafsi

Waziri Dkt. Ndumbaro Aielekeza Bodi ya Filamu Kushirikiana na Sekta Binafsi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameilekeza Bodi ya Filamu nchini ishirikiane na Sekta binafsi katika kuhakikisha filamu za Tanzania zinakua bora zaidi na zinapata soko la uhakika.

Dkt. Ndumbaro ametoa agizo hilo Oktoba 12, 2023 alipofanya ziara katika Bodi hiyo, ambapo ameitaka iendelee kudhibiti na kufanya uhakiki wa ubora wa Filamu ili kulinda Mila na desturi za Tanzania.

Ameitaka Bodi hiyo ibadilike na kwenda na wakati Ili kupanua wigo wa kuwahudumia wadau wake kibiashara na kuongeza mapato.

F8T5aeBWMAAJHh7.jpg
F8T5aw_WUAA_G2D.jpg
F8T5b2UXgAA7uW2.jpg
F8T5ePxXsAAHcEy.jpg
 
Back
Top Bottom