Waziri Dkt. Ndumbaro Akutana na Waziri wa Michezo wa Misri

Waziri Dkt. Ndumbaro Akutana na Waziri wa Michezo wa Misri

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WAZIRI DKT. NDUMBARO ATETA NA WAZIRI WA MICHEZO MISRI

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Vijana na Michezo wa nchini Misri Mhe. Ashraf Sobh Septemba 25, 2023 Jijini Cairo.

Viongozi hao wamekubaliana kushirikiana baina ya nchi hizo mbili hususan kubadilishana uzoefu na kutoa mafunzo katika Sekta ya michezo.

Aidha, Waziri na ujumbe wa Tanzania walipata wasaa wa kutembelea Kituo cha michezo cha Algazira Club ambacho kina viwanja mbalimbali vya kulea vipaji vya michezo kuanzia watoto wadogo hadi vijana ambao ni hazina kubwa ya wanamichezo katika taifa.

Katika ziara hiyo, Mhe. Dkt. Ndumbaro aliambatana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo (BMT) Bi Neema Msitha, Mwenyekiti wa Baraza hilo Ndg. Leodigar Tenga, baadhi ya viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania pamoja na watumishi wa Wizara hiyo.​

 

Attachments

  • F671SdvWAAAokW-.jpg
    F671SdvWAAAokW-.jpg
    103 KB · Views: 3
  • F671S5iXEAAVitZ.jpg
    F671S5iXEAAVitZ.jpg
    102.1 KB · Views: 2
  • F671TVgWMAA_7Ju.jpg
    F671TVgWMAA_7Ju.jpg
    92.6 KB · Views: 2
  • F671TtwXsAAxtTu.jpg
    F671TtwXsAAxtTu.jpg
    91.9 KB · Views: 3
Back
Top Bottom