Waziri Dkt. Ndumbaro asisitiza wadau kushirikiana na Serikali kuendeleza Michezo Nchini

Waziri Dkt. Ndumbaro asisitiza wadau kushirikiana na Serikali kuendeleza Michezo Nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
WAZIRI DKT. NDUMBARO ASISITIZA WADAU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUENDELEZA MICHEZO NCHINI

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Septemba 20, 2023 Jijini Dar es Salaam amekutana na viongozi wa timu ya Simba ambapo wamejadili masuala mbalimbali yakiwemo maendeleo ya michezo nchini.

Kikao hicho pia kimejadili maandalizi ya michuano ya Africa Football League ambayo timu ya Simba inashiriki ikiwa miongoni mwa timu nane bora Afrika.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Ally Mayayi, Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha, Katibu wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini Bw. Wilfred Kidau, Mtendaji Mkuu wa Timu ya Simba Bw. Iman Kajula pamoja na viongozi wengine.

F6egb_2XwAAe0jb.jpg

F6egce1WQAEGaUn.jpg

F6egctsWoAAz65N.jpg
F6egdTdWoAA1cp5.jpg
 
Back
Top Bottom