Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro amesema Tanzania imeandaa mashindano mapya yaliyopewa jina la ‘Mwalimu Nyerere Liberation Cup’ ambayo yatakuwa ni mashindano ya vijana wenye umri wa miaka 20 yatakayojumuisha Bara lote la Afrika.
Dkt. Ndumbaro amesema hayo katika ufunguzi wa mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Mashindano ya Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) kwa ngazi ya taifa, kwa mwaka 2024 yaliyofanyika mkoani Tabora.
“Tutaweka michezo ya aina mbalimbali na sisi Tanzania ndio wenyeji kwa hiyo vijana watakaotoka kwenye mashindano haya (UMITASHUMTA na UMISSETA) watahusika katika kombe hilo,” ameongeza Dkt. Ndumbaro.