Waziri Dkt. Stergomena aonya uvamizi wa maeneo ya jeshi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) awasili Mkoani Mtwara kutatua kero ya mgogoro wa ardhi kati ya Kikosi cha Jeshi 665 Regt na Wananchi wa Mbae Mashariki eneo ambalo limevamiwa na kujengwa makazi.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika mkutano huo, Dkt. Steromena amesema kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anayo dhamira ya dhati kuhakikisha migogoro ya ardhi nchini inamalizwa.

Aidha Mhe. Dkt. Stergomena alipata fursa pia kutembelea maeneo yote ya mgogoro na kuzungumza na Wananchi waishio eneo hilo.

Vilevile amewasihi wananchihao kuacha kuvamia eneo hilo kwani ni hatarishi kutokana na eneo hilo kuwa maalum kwa matumizi ya Kijeshi.

Naye Mbunge wa Mtwara Mjini, Mhe. Selemani Mtenja amemshukuru Dkt. Stergomena Tax kwa juhudi na utashi wa kutatua mgogoro huo, kwani amekuwa Waziri wa kwanza kutembelea eneo la mgogoro na kuzungumza na wananchi kwa lengo kupata suluhu.

 
Na jeshi wanavamia maeneo ya wananchi uijue hilo vile vile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…