Waziri Dkt. Stergomena atembelea Mradi Ujenzi Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa

Waziri Dkt. Stergomena atembelea Mradi Ujenzi Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
2.JPG

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax ametembelea Mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa eneo la Kikombo, wilaya ya Chamwino Dodoma, tarehe 12 Julai, 2022.

Hii ni ziara ya pili kwa Waziri kutembelea mradi wa ujenzi. Lengo la ziara hiyo, ni kukagua na kujionea hatua za maendeleo ya ujenzi unaotekelezwa kwa Force Account kwa kutumia wataalamu wa ndani.

Mpaka sasa ujenzi wa maradi huo, ziara ya kwanza ya Waziri kutembelea ujenzi huo ilikuwa ni tarehe 28 Septemba, 2021.
4.JPG

Baada ya kutembelea na kupatiwa maelezo ya kina kuhusu utekelezaji wa mradi huo, Dkt. Stergomena amepongeza na kusifu kazi kubwa na nzuri inayoendelea kufanywa na kikosi kazi hicho, kwani ujenzi huo umefikia hatua nzuri.

“Kama ilivyoelezwa katika maelezo ya awali, hii ni mara yangu ya pili, nilipokuja na nilipokuja leo nimeona mabadiliko makubwa sana. Naomba nianze kwa kutoa pongezi kubwa kwa kazi kubwa inayoendelea kufanywa, maana hapa tulipofikia, tumefika mahali pazuri sana.

"Hii inathibitisha kuwa wanajeshi wanaweza kila kazi, na hakuna kazi inayoweza kufanywa na mwanajeshi ikashindikana,” alisema.
5.JPG

Akitoa maelezo ya utangulizi kwa Waziri, Msimamizi Mkuu wa mradi huo, Meja Jenerali Hawa Kodi amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo, umeanza tangu tarehe 20 Machi, 2020 na unatarajiwa kukamilika ifikakapo tarehe 22 Oktoba, 2022 ambapo umefikia asilimia 92.

Utapokamilika utakuwa umegharimu takriban Shilingi 58.5 iwapo ungetekelezwa na Mkandarasi kutoka nje ungegharimu takriban shilingi bilioni 127.19 na kuokoa zaidi ya Shilingi bilioni 68.7

Naye, Kanali Zabron Mahenge akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya mradi kabla ya Dkt. Stergomena kutembelea na kukagua jengo na kujionea hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi huo.

Amesema kuwa Makao Makuu hayo kwa pamoja yatakuwa na ofisi 1032 na yamegawanyika katika maeneo Makuu matatu ambapo eneo la Kwanza litakuwa na ofisi za Wizara ya Ulinzi na JKT kwa upande wa magharibi, eneo la Pili litakuwa na Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi upande wa mashariki na eneo la Tatu litakuwa na ofisi za Wakuu wa Kamandi chini ya JWTZ kwa upande wa nyuma.

Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa ulizinduliwa kwa kuwekewa jiwe la msingi na aliyekuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano na Amiri Jeshi Mkuu, Hayati John Pombe Joseph Maguli tarehe 25 Novemba, 2019 ambapo alitoa shilingi Bilioni 10 kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa.
 
Sioni umuhimu wa kuhamia Dodoma ni kutumia pesa za walipa kodi vibaya! Tz tuna vipaumbele muhimu kuliko kujenga majengo mapya Dodoma
Hata makao makuu yangebaki Dar msingekosa la kuongea, kuwa kiiiiila kitu nchi hii Dar, ili kuondoa maneno wakaamua makao makuu yaende kati ya nchi.

Sasa endeleeni kuropokwa
 
Baada ya jengo kukamulika hapo nje ya hilo jengo wa design kitu flan cha ki militaire kama kombora iwe kama kivutio au waweke sanamu la nyerere au crown kubwa ya JWTZ itapendeza sana
 
Baada ya jengo kukamulika hapo nje ya hilo jengo wa design kitu flan cha ki militaire kama kombora iwe kama kivutio au waweke sanamu la nyerere au crown kubwa ya JWTZ itapendeza sana
Kivutio cha nini unadhani hilo jumba ni LA 'royo tua'?
Nyerere wa kazi gani,vyote alivyopewa nchi hii havimtoshi?
Kwenye crown LA jwtz hapo sawa.
 
Back
Top Bottom