Waziri Dkt. Stergomena azungumzia kujivunia timu ya Wacheza Golf Wanawake

Waziri Dkt. Stergomena azungumzia kujivunia timu ya Wacheza Golf Wanawake

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
6_Easy-Resize.com (1).jpg

1_Easy-Resize.com (3).jpg

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Stergomena Lawrence Tax (Mb) amesema kuwa anayo mengi ya kujivunia kwa timu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Golf ya Wanawake (TPDF Lugalo Golf Club) yakiwemo ya kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi. Timu hii imeendelea kufanya vizuri kwa kuibuka washindi inapocheza na timu za ndani na hata zile za nje ya nchi.

“Yapo mengi ya kujivunia katika klabu hii, hasa Timu ya Gofu ya Wanawake. Kweli Timu hii inaitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi na hasa inapocheza nje ya nchi. Mliweza kushinda mlipoenda kucheza Nigeria, mliweza kushinda mlipoenda kucheza Ghana, mliweza kushinda mlipoenda kucheza Kenya, na mliweza kushinda mlipoenda kucheza Uganda. Na mmeweza kutoa mchango mkubwa kwa Timu ya Taifa,” alisema.

Tax ameyasema hayo wakati akiwa Mgeni Rasmi wakati wa kufunga Mashindano ya Lugalo Ladies Open 22 yaliyofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 21 – 22 Mei, 2022 katika Viwanja TPDF Lugalo Golf Club, mashindano yaliyozishirikisha Timu sita, Timu mbili kutoka kila mkoa kwa mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Kilimanjaro.

Akiongea maneno ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kuongea na wageni waalikwa, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amesema kuwa mashindano haya yamepangwa na kuratibiwa na wanawake wenyewe. “Kiukweli hadi kufanikiwa kwa mashindano haya wanawake wenyewe wameanzisha, wamejipanga hadi kusimamia mashindano haya,” alisema.

Dkt Stergomena amewapongeza washiriki wa mashindano hayo kwa ushiriki wao na kwa namna walivyohamsika na kuamua kushiriki kwa wingi licha ya majukumu mengi yanayowakabili.

Vilevile ameupongeza uongozi wa TPDF Lugalo Golf Club kwa jitihada zake za kuiunga mkono pamoja na kuibua vipaji kwa wanawake.

Pia, Waziri amewapongeza washiriki walioibuka washindi na kutunukiwa zawadi mbalimbali zikiwemo vikombe, tiketi za ndege na Fridge. Kwa kuwa michezo ni burudani, amewasihi wale wote ambao hawakufikia ushindi wasikate tama bali waendelee kushiriki. Aidha, amewashukuru wadhamini kwa kuona umuhimu wa kudhamini na hatimaye kufanikisha mashindano hayo.

Mbali na kufunga mashindano hayo Waziri aliongoza Harambee ya kuchangia Mfuko wa Wanawake wa Wacheza Gofu ambapo yeye binafsi aliweza kuchangia shilingi milioni 25 taslimu ili kuiwezesha timu hiyo kushiriki mashindano yatakayofanyika mwezi Septemba mwaka huu nchini Kenya.. Aidha, ameahidi kuendelea kuisaidia timu hiyo kwa kadri atakavyoona inafaa. Pia, amezitaka timu za wanaume nazo zijitahidi kufanya vizuri ili kuitia moyo timu ya wanawake wachezag gofu.

Mashindano hayo yamedhaminiwa na makampuni mbalimbali na watu binafsi yakiwemo QatarAir, Akiba Commercial Bank,PrecionAir, GreatLakes, sana, SBC (Pepsi), Angels, Serena Hotels, Mohammed Enterprises Limited, Johnie Walker na 24/7 Adventure.
3_Easy-Resize.com (3).jpg
 
Wizara imemtosha huyu mama hadi naona raha ,sijui wizara angepewa Nape sa hivi ingekuwaje?

Rais Mwinyi, Hayati Kwendeka na Sasa mama Tax wameonesha busara na wizara hii iwe kipimo cha kupata viongozi wa juu.
Haijamtosha hata. Mawaziri wa wizara hii huwa hawana muda na kamera na waandishi wa habari. Huwa wapo kama hawapo.
 
Wizara imemtosha huyu mama hadi naona raha ,sijui wizara angepewa Nape sa hivi ingekuwaje?

Rais Mwinyi, Hayati Kwendeka na Sasa mama Tax wameonesha busara na wizara hii iwe kipimo cha kupata viongozi wa juu.
Nape hata baba yake kule vitani UG alipewa tu mic hakupigana Vita,like father like son, Kuna watu vitu Fulani sio vya kuwapa, Hata Nape alifaa kuwa CCM sio serikalini
 
Wizara imemtosha huyu mama hadi naona raha ,sijui wizara angepewa Nape sa hivi ingekuwaje?

Rais Mwinyi, Hayati Kwendeka na Sasa mama Tax wameonesha busara na wizara hii iwe kipimo cha kupata viongozi wa juu.
Kweli mkuu.
 
Uliwahi kumuona Mwinyi Rais wa Sasa wa Zanzibar kwenye macamera macamera kipindi ni waziri wa ulinzi?🤔
 
Back
Top Bottom