WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, nchini Tanzania Dk. Dorothy Gwajima amewaacha na hamaki wakazi wa jiji la Mwanza mara baada ya kusema, baada ya yeye kuchanja chanjo ya UVIKO-19, mume wake ametesti ‘mitambo’ kwake na kukuta yupo ‘fiti’ kama mwanamke.
Ametoa kauli hivyo jana jijini Mwanza alipokagua jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sekou Toure ya Jijini Mwanza. Amesema chanjo haiathiri kitu chochote katika mwili ndio maana yeye yupo vizuri baada ya kuchanjwa chanjo hiyo na kuhimiza watu kwenda kuchanjwa, “Hakuna aliyechanjwa akageuka kuwa zombi.”
Mtu mwenye dhamana ya Waziri bila shaka anatakiwa kuwa makini kwenye matamko mbalimbali, kutoa kauli kama hii ya mambo ya faragha kati yake na mume wake, hata kama ni kwa kuhamasisha watu wakachanjwe chanjo ya COVID 19 kauli ya namna hii siyo nzuri amemwaibisha mume wake na amejiaabisha mwenyewe kwa hadhi aliyonayo.
Kauli hiyo haiwezi kuleta ushawishi wowote wa kuwafanya watu waitikie kupata chanjo hiyo, nafikiri ni vyema kamati za maadili na viongozi wastaafu kukaa na viongozi wa namna hii na kuwaonya kutokutumia kauli za aina hii maana hazifai.
Hivi kama mume wake angetest akakuta kuna mabadiliko ikatokea tafrani kati yao angeutangazia umma wa wa Tanzania jambo hilo?
Au kulikuwa na ulazima gani wa kutamka maneno ya aina hiyo?
Ni hayo tu, karibuni wadau na ninyi mtoe maoni yenu juu ya kauli hii ya mh waziri.