#COVID19 Waziri Gwajima aagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19

Mimi nilidhani ni mtu na dada yake kumbe ni mtu na shemejiye!
Mie nasubiri hio ligi vile itakavyo kuwa.
 
Hicho kichaka hakitakusaidia sana, tuambiwe, madhara (side effects) za hizo chanjo baada ya miaka mi5 ni zipi? Kwa atakayechomwa na kwa watoto atakaowazaa, ziwekwe wazi na watuambie walifanya hayo majaribio kuanzia mwaka gani hadi mwaka gani...
Google basi dogooooo
 
Jameni mwacheni Doroth aupige mwingi.

Alishasema vita hupiganwa kwa silaha ya wakati husika.

Kinjekitile alitumia silaha ya maji, japo ilikuwa imani potofu, akajitutumua kushindana na mjerumani aloyekuwa na bunduki. Anyway, hiyo ndiyo silaha waliyoimudu wakati wao.

Enzi za mwendazake Jiwe tulipewa malimao, pilipili kichaa, tangawizi, miarobaini, nk, kwani ndiyo silaha zilizokuwepo.

Dunia imetengeneza silaha mpya (SMG) chanjo, sisi ni nani mpaka tusinunue silaha mpya tuupige mwingi?

Nasimama na Doroth...
 
Najiuliza je ni kweli kwamba mwwchama wa ccm ambaye atachaguliwa ama kuteuliwa nafasi ya uongozi wa juu wa chama cha mapinduzi hafanyi kiapo cha utii kwa viongozi wao wakuu na hata kwa chama kabla ya kukabidhiwa wadhifa husika? na kama ndiyo je hawa wanaopingana na viongozi wao kwa habari ya chanjo wanapta wapi ujasiri? na chama kinawachukulia hatua gani za kwadhibiti ama kuwaadhibu kwa utovu wa nidhamu kwa chama na kwa viongozi wakuu kabla hawajasababisha madhara makubwa zaidi kwenye chama na kwa taifa?

kwa mfano kama mbunge wa chama kinachotawala anaweza kusimama hadharani akampinga mwenyekiti wake wa chama ambacho ndicho kilichompatia ridhaa ya uongozi huu ni sawa kukosa adabu na kuondokewa kwa utii kulikopitiliza na hii ni dharau sana kwa kiongozi wako mkuu wa chama chako

lakini kwa sababu mtu huyu siyo mwenye madaraka ya mwisho kwenye chama ni bora kamati kuu ya chama wakakaa kwa ajili yake na kumjadili mwisho wa siku wafikie mahali wakubali kumfuta uanachama kwenye chama jambo ambalo litakalomsababisha mtu huyo pia kukosa ama kupoteza sifa ya kuendelea na uongozi Kwenye nafasi ambazo amezipata kupitia chama ama ambazo sifa ya kuzipata ni kuwa mwanachama wa chama husika

ikiwa hivyo watu ama viongozi watakumbuka kuwaheshimu na kuwatii wakuu wao ktk madaraka.
 
Moja ya AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko
 
Huyu waziri atapelekewa moto na mchungaji gwajima hadi aombe poo
Mda huu tayari Gwajima yupo busy kusaka siri zake udhaifu wake wote mapungufu yake yote apate kuyaanika kwa ile style ya kuliamsha dude
 
"Hatujapa taarifa rasmi ya maandishi ya kutakiwa kumkamata Mhe.Gwajima, lakini hata tukiipokea tutachunguza iwapo matamshi yake yanaangukia Kwenye Jinai, lakini tunaweza kuwashauri wakatatua jambo hili kwa njia za mazungumzo badala ya Polisi"-IGP Simon Sirro

 
It's a War against two idiots.
They used to worship the same god mwendazake, but now everyone is looking for his/her own 🍞 bread
A bread is now became their god
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…