#COVID19 Waziri Gwajima aagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19

#COVID19 Waziri Gwajima aagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19

Waziri nae abaki na ya kaizari, asiingilie mambo ya wenye Imani . Kumwambia mwenye Imani athibitishe maana yake anataka Mwenyezi-MUNGU athibitishe. Mwenyezi MUNGU akiamua waliochoma chanjo wapate madhara waziri anayotaka Askofu Gwajima athibitishe ,atawezana.
 
gwajimapicc.jpeg
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima ameliagiza Jeshi la Polisi pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini ( Takukuru) kumkamata na kumhoji mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya Uviko 19.

Dk Gwajima ametoa agizo hilo leo Jumanne Agosti 17, 2021 katika kijiji cha Kyatunge wilayani Butiama akibainisha kuwa Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi jambo linaloivuruga wizara yake na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo. (Mwananchi)
 
Duh.
Waziri Dr. Doroth Gwajima amekosea kuagiza polisi na TAKUKURU wamkamate Askofu Josephat Gwajima.

Kama kuna jinai zilipaswa mamlaka husika zianze uchunguzi na kisha hatua za kisheria hata kabla ya kuagizwa.

Tusikubali kurudi kwenye utawala wa maagizo. Tuheshimu uhuru wa maoni na utawala wa sheria.

Tunataka Katiba Mpya.
 
Waziri nae abaki na ya kaizari,asiingilie mambo ya wenye Imani . Kumwambia mwenye Imani athibitishe maana yake anataka Mwenyezi-MUNGU athibitishe. Mwenyezi MUNGU akiamua waliochoma chanjo wapate madhara waziri anayotaka Askofu Gwajima athibitishe ,atawezana

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
Ndio athibitishe tuu shida iko wapi? Then kama yete hataki chanjo maneno mengi yanini?
 
Rais hawezi kusoma ripoti, kuwaza nje ya boksi acha apelekeshwe. How come anasema Tanzania ni nchi jirani na marekani? unaona kuna mtu humo mkuu.
 
Andika Gwajima ataka Gwajima mwingine akamatwe
 
Josefu alikua akiongelea mambo ya kiroho' Dorothy anaongela mambo ya kimwili. Hau gwajilady amesahau kuwa kanisa la gwajiboy linafufua na kutoa uzima?
Ameshafufua wangapi hadi sasa? Kwanini ameshindwa kuwafufua ukoo wake?
 
Kujiita askofu ni kuchafua hadhi ya uaskofu, kuwa askofu kuna kanuni zake sio kujitangazia kiholela. Kamati iliyokaa na kumpa Gwagima uaskofu waliangalia sifa za uaskofu? Bila shaka hawakuangalia ndio maana anapayuka ovyo. Chungu ulimi wako mbele ya serikali.
Askofu wa kweli ni yupi? Anaye valia kofia na fimbo?
 
Back
Top Bottom