#COVID19 Waziri Gwajima aagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19

#COVID19 Waziri Gwajima aagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19

Kwani ni lazima mtangaze kukamatwa kwake? Kamchukueni kimya kimya kama ilivyofanyika kwa mbowe.
 
Butiama.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima ameliagiza Jeshi la Polisi pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini ( Takukuru) kumkamata na kumhoji mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya Uviko 19.

Dk Gwajima ametoa agizo hilo leo Jumanne Agosti 17, 2021 katika kijiji cha Kyatunge wilayani Butiama akibainisha kuwa Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi jambo linaloivuruga wizara yake na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Credits: Mwananchi

Pia soma
- #COVID19 - Dkt. Mollel: Askofu Gwajima ataitwa athibitishe kauli zake, akishindwa tutamshughulikia
Taasisi kupambana na Rushwa inaingiaje hapo?! kwani kuna pesa klitolewa kwake akaitafuna.!
Itumieni taasisi hii kwa jinsi ya majukumu yake. Tusipotoshe ukweli.
 
Waziri wa afya Dkt Dorothy Gwajima aliagiza jeshi la polisi kumkamata Mbunge mh Gwajima kwasababu anapotosha umma pia amesema anayumbisha wizara yake.

Screenshot_20210817-152659.png
 
waziri wa afya dk doros gwajima aliagiza jeshi la polisi kumkamata mbunge mh Gwajima kwasababu anapotosha uma pia amesema anayumbisha wizara yake.

Huyu ni nabii kwa mujibu wa madai yake.

Kama Paulo na Sila, tusubirie milango ya gereza kufunguka.
 
Kujiita askofu ni kuchafua hadhi ya uaskofu, kuwa askofu kuna kanuni zake sio kujitangazia kiholela. Kamati iliyokaa na kumpa Gwagima uaskofu waliangalia sifa za uaskofu? Bila shaka hawakuangalia ndio maana anapayuka ovyo. Chungu ulimi wako mbele ya serikali.
Unashangaa Gwaji kuwa askofu?
Hebu njoo huku lidazi umuone bishop Mkandamizaji anachunga kundi la kondoo wa Bwana, yaani ni full comedy 😂😂
 
Kimsingi akamatwe tu,km ana msimamo wake abaki nao tu sio kila siku kuhubiri juu ya huo msimamo,kila mtu anabega lake la kuchanja,huyu ni mkwamishaji,mpotoshaji kama wapotoshaji wengine,anavyoachwa hivi sio afya kwa wizara na mapambano ya Uviko-19
 
*NITAKUUMBUA" ni maneno aliyosema gwajima wiki zilizopita kwa yeyote ataetala kupingana nae hoja.

Wacha tusubiri
 
waziri wa afya dk doros gwajima aliagiza jeshi la polisi kumkamata mbunge mh Gwajima kwasababu anapotosha uma pia amesema anayumbisha wizara yake.

View attachment 1895637
Amefanya kosa gani kisheria? Mbona huyo naibu waziri na waziri wake ndio walikuwa wanatuambia tupige nyungu?
Gwajima akikamatwa nitaamini kwamba nyuma ya hii chanjo kuna agenda ya siri
 
Amefanya kosa gani kisheria? Mbona huyo naibu waziri na waziri wake ndio walikuwa wanatuambia tupige nyungu?
Gwajima akikamatwa nitaamini kwamba nyuma ya hii chanjo kuna agenda ya siri
Yaani waziri anataka kupangia watu vya kuongea kwenye mimbari za nyumba za Mungu!
Mama Samia hii wizara haina msaada kwako. Imegeuka kuwa wana siasa tu.
 
Wameshatoa enough data

Ni wakati sasa gwajiboy athibitishe tuhuma dhidi ya chanjo feki, content ya chanjo na madhara ya chanjo
Gwajima kapewa nafasi ya kuthibitisha asilie lie uwanja Ni wake akathibitishe kuwa chanjo inasababisha watu wawe mazombi
 
Back
Top Bottom