#COVID19 Waziri Gwajima aagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19

#COVID19 Waziri Gwajima aagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19

Taasisi kupambana na Rushwa inaingiaje hapo?! kwani kuna pesa klitolewa kwake akaitafuna.!
Itumieni taasisi hii kwa jinsi ya majukumu yake. Tusipotoshe ukweli.
Kama Gwajima aliwatuhumu watu kuwa wamepata kitu kidogo hapo Basi Takukuru watamuomba athibitishe hizo tuhuma
 
  • Thanks
Reactions: Mj1
Mtu na shemejie..😂
Tanzania hatujafikia kiwango hicho cha demokrasia na hata uelewa wa siasa katika jamii bado sana tusijeshangaa mume wa Gwajima (Dr) akimnunia mkewe (Kama sio kumtaliki), wakwe zake Dr. kama wapo wataacha laana za kufa mtu kwa kumfunga kaka/mtoto wao............ (Kama akifungwa) ........

Kopo langu la popukoni liko wapi mwanawane.................
 
Wampeleke mahabara ya taifa kwenye kila aina chemical na kifaa atakachohitaji kwenye test zake athibitishe madai yake ili asiseme kaonewa bila ya kusahau na kichupa kimoja cha vaccine.

Akifika huko achanganye hayo madawa mbele ya camera kuthibitisha madai yake kwa umma nini kimo ndani hiyo vaccine kama anavyodai.

Bishop Gwajima anavuka mipaka yake.
Gwajima akachanganye madawa ana leseni ya kufanya hivyo?
 
Hahaha huyu maza anachemka, hii sio namna bora ya kupambana na Gwajiboy, hawaoni anaungwa mkono na wananchi wengi?
Hata Mbowe anaungwa mkono na wananchi wengi lakini amekamatwa!

Acha wakamatwe kamatwe hovyo ili mwisho wananchi wakikosa wa kuwasemea mambo yao watasema wenyewe kwa vitendo...

Tuendelee kula mtori nyama tutazikuta chini
 
Umenena! Anaevaa kofia na fimbo ndio wenyewe! Wamepikwa kifalsafa wakaiva ndio maana kamwe husikii matusi kutoka vinywa vyao. Usione wapo kimya, ndivyo walivyo, leta hoja wakujibu kifalsafa.
 
Gwajima akachanganye madawa ana leseni ya kufanya hivyo?
Leseni hiyo hiyo aliyotumia kutoa expert opinion ya kuwa dawa ni maji, sijui zimewekewa nini aruhusiwe kuendelea nayo kwenye kuthibitisha.

Aende kuchezea centrifuge huko maabara na test tube kuthibitisha madai yake. Yeye si anajua sana nini kimo ndani ya hizo vaccine kushinda wataalamu wa afya.

Serikali itajibu vipi madai yake bila ya yeye kuthibitisha kwanza uhalali wenyewe.

Gwajima asipotokea itatufanya tumuone muongo kweli kweli.
 
Askofu Gwajima ni shemeji yangu, lakini mimi waziri wa wananchi nimekula kiapo mbele ya Rais cha kutumiakia nchi, sio kumtumikia shemeji. Mimi ndiye msemaji wa masuala ya afya nchini, nimechoka kuvurugwa naagiza akamatwe popote na akahojiwe juu ya haya madai - Dk. Gwajima
Dorothy anavurugwa au ashajivuruga kupitia vitunguu na mivumbasi ya kuijvukizia?

Huyu mama kivuruge kweli
 
Baada ya askofu Gwajima kukamatwa na Takukuru ni vema akahojiwa na jopo la wanasayansi ili baada ya hapo mjadala ufungwe rasmi tuendelee na majukumu mengine

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Kwanini wasimuite huko bungeni kama walivyomfanyia ndugu yetu mayala a.k.a Njaa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Nchi imekuwa ya kipuuzi kweli kweli.

Hawa wapumbavu mawaziri wa Afya wenyewe, pamoja na huyo askofu wanatakiwa kukamatwa na kuwekwa ndani kwa upuuzi waliowafanyia waTanzania tokea mwanzo wa ugonjwa huu.
 
Ulijivuruga mwenyewe uliposema kuwa surua imeisha kwa kuchemsha mwarobani na sala.

That was the end of your legitimacy
 
Baada ya askofu Gwajima kukamatwa na Takukuru ni vema akahojiwa na jopo la wanasayansi ili baada ya hapo mjadala ufungwe rasmi tuendelee na majukumu mengine

Mungu ni mwema wakati wote!
Yeye mwenyewe hawe ku prove hojq zake kisayansi. why wapambane nae wkt hana utaalqm wowote?
 
Askofu Gwajima ni shemeji yangu, lakini mimi waziri wa wananchi nimekula kiapo mbele ya Rais cha kutumiakia nchi, sio kumtumikia shemeji. Mimi ndiye msemaji wa masuala ya afya nchini, nimechoka kuvurugwa naagiza akamatwe popote na akahojiwe juu ya haya madai - Dk. Gwajima...
Hii nchi kila Waziri ana mamlaka ya kuruhusu mtu kukamatwa kwa sasa.
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Back
Top Bottom