#COVID19 Waziri Gwajima aagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19

#COVID19 Waziri Gwajima aagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19

Ni wazi IGP Sirro ameshaogopa kumkamata Askofu Gwajima na IGP ni CCM damu damu, bila aibu anasema eti "tutawashauri watatute jambo hili kwa njia ya mazumgumzo".

Mbona hajawahi kuwashauri wapinzani kutatua matatizo kwa njia ya mazungumzo, huwa anatoa vitisho na kuwakamata kwa nguvu.

Yeye mtu wa CCM anaezua taharuki kwa wananchi na kupinga serikali wazi wazi anamshauri kutatua kwa njia ya mazungumzo, ila mtu anaedai katiba mpya kwa njia ya amani ni adui na wakukamatwa kwa kutumia mabomu ya machozi na nguvu nyingi.

Yupi ni mtu hatari, anaezua taharuki na kupotosha taifa au anaedai katiba ya nchi yake kwa njia ya amani???
 
Ni wazi IGP Sirro ameshaogopa kumkamata Askofu Gwajima na ni CCM damu damu,, bila aibu anasema eti "tutawashauri watatute jambo hili kwa njia ya mazumgumzo".

Mbona hajawahi kuwashauri wapinzani kutatua matatizo kwa njia ya mazungumzo, huwa anatoa vitisho na kuwakamata kwa nguvu.
Polisi ni jibwa, lenye ufahamu linalojitoa fahamu, inategemea lumetumwa kwa Nani
 
Huyu Padre wa CCM na mbunge wa kura za wizi Gwajima anakivuruga chama na kukigawa mapande, zarau za padoro huyu zimevuka mipaka na sasa ameanza kuota mapembe kwa kusema yupo tayari kupoteza, ubunge, dongo hili wamepigwa wakuu wa chama, inaonekana hata Siro ameelemea upande wa Gwajima kwa kukataa amri ya kumkamata, hili nalo linatoa viashiria kuwa Gwajima hayupo peke yake anawatu wanaompa jeuri,ni umoja au mtandao unaopinga juhudi za Raisi Samia.

Hawa polisi walikuwa wanapokea amri za wakuu wa wilaya na hata madiwani,leo polisi wanadai barua ,sasa tuseme Jeshi la Polisi limeanza kufuata sheria?

Tunasubiri vikao vya Chama kumdhibiti Padiri Gwajima ,Je Mashaka Hamidu Mashaka ataweza ?
 
Huyu Padre wa CCM na mbunge wa kura za wizi Gwajima anakivuruga chama na kukigawa mapande, zarau za padoro huyu zimevuka mipaka na sasa ameanza kuota mapembe kwa kusema yupo tayari kupoteza, ubunge, dongo hili wamepigwa wakuu wa chama ,inaonekana hata Siro ameelemea upande wa Gwajima kwa kukataa amri ya kumkamata,hili nalo linatoa viashiria kuwa Gwajima hayupo peke yake anawatu wanaompa jeuri,ni umoja au mtandao unaopinga juhudi za Raisi Samia.
Hawa polisi walikuwa wanapokea amri za wakuu wa wilaya na hata madiwani,leo polisi wanadai barua ,sasa tuseme Jeshi la Polisi limeanza kufuata sheria ?
Tunasubiri vikao vya Chama kumdhibiti Padiri Gwajima ,Je Mashaka Hamidu Mashaka ataweza ?
Rekebisha,
Gwajima sio Padre
 
Sirro yupo sahihi maana Nadhani pro JPM wanajiandaa kujikusanya na kiunganishi kinaweza kuwa Gwajima. Kitendo cha Mbowe kwenda kudai katiba mpya mwanza-usukumani ni kujaribu karata yake maana 2025 pro JPM ndiye Rais. Najua Mshana Jr utanipinga lakini haya ni mahesabu mazito
 
Bro umeunganisha dots,hii vita sio ndogo ,CCM wenyeviti wasipoangalia akina Gwajima gangs watapindua meza wanauwinda uraisi 2025 na hiiki anachokifanya Gwajima ni kuzidi kwa wao kujipambanua na hisia zinaonyesha ,kufikia Siro kudai barua kwa Waziri ambae ni mteule wa Raisi,Team Gwajima inaanza kuota pembe.
 
Sirro ana inteligensia kumbuka na yupo royal kwa Samia
 
Chief kaa chini tena ikiwezekana ingia darasani ukasome. We umeona wapi mtu aliyeko kwenye Local government (Serikali za mitaa) ana mamlaka kuliko aliyeko kwenye Central govenment? (Serikali kuu)
Hao wakuu wa mikoa wote wako chini ya waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa tofauti na mawaziri wote wengine.
Ciao! [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji125][emoji125][emoji125][emoji377][emoji377][emoji377]
Watanzania wengi husoma ila hawawaelimiki
 
Waziri wa afya ana mamlaka ya kuamrisha jeshi la polisi? Hii nchi inaongozwa na vilaza watupu
Wewe ndye kilaza waziri ni mwakilishi wa rais ndyo maana anatembea na bendera ya taifa kwenye gari yake
 
Je atakamatwaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji779]???
Sirro kagoma kumkamata, anasema mpaka apate barua ya maagizo.
Imagine angekuwa ni Lissu ama Lipumba, limetolewa tamko la namna hiyo, tungekuwa tunaongea habari gani leo?
 
Waziri wa afya ana mamlaka ya kuamrisha jeshi la polisi? Hii nchi inaongozwa na vilaza watupu
Kama kuna mtu anatoa habari potofu kuhusu afya za Watanzania waziri wa afya ana jukumu la kuomba vyombo vya usalama viingilie. Hiyo ndiyo coordination kwenye serikali, wizara zinafanya kazi pamoja.
 
Kama kuna mtu anatoa habari potofu kuhusu afya za Watanzania waziri wa afya ana jukumu la kuomba vyombo vya usalama viingilie. Hiyo ndiyo coordination kwenye serikali, wizara zinafanya kazi pamoja.
Mbona wamemgomea?
 
Kama kuna mtu anatoa habari potofu kuhusu afya za Watanzania waziri wa afya ana jukumu la kuomba vyombo vya usalama viingilie. Hiyo ndiyo coordination kwenye serikali, wizara zinafanya kazi pamoja.

Eti vyombo vya usalama?!

Mbona vina majukumu yake ya kawaida tu ya kutimiza !

Kwanini mpapenda kutishana na kuadhibiana?

Kama kuna mtu anapotosha jambo njia Nzuri ni yule mwenye ukweli kujitokeza hata kwa njia ya kuongea na waandishi wa Habari na kusema “ jamani kuna taarifa fulani siyo sahihi hebu zipuuzeni ni upotoshaji, ukweli ni huu na huuu “

Lakini mambo ya kutishiana kukamatana na ubabe vitawasadia nini?!
 
Back
Top Bottom