Waziri Gwajima: Alichofanyiwa binti wa Yombo ni kitendo kibaya kisicho na utu, nimewasiliana na Waziri wa Mambo ya Ndani ili haki itendeke

Waziri Gwajima: Alichofanyiwa binti wa Yombo ni kitendo kibaya kisicho na utu, nimewasiliana na Waziri wa Mambo ya Ndani ili haki itendeke

TUNALINDANA.tunaomba hili lisipite kimya kimya hawa polisi wanataka kutugeuza mabwege.wapelekwe mahakamani. Ndo hukumu ikatoke kuwa wavuta bangi na malaya.ila sio yeye polisi atuambie huo utumbo.
 
Tayar mkuu
Alikngea akiwa amelewa!
20240819_140603.jpg
 
Safi sana Mama Gwajima,Kuzima makali ya kesi Geshi linamuita binti malaya kutupumbaza kisaikolojia.Kwa utamaduni wa watu wachache wenye akili fupi kuitwa malaya tayari ni kuwalinda wabakaji mmoja wapo ni mwanajeshi wa Jeshi la wananchi na picha yake ipo wazi hata humu JF.Kwanini Afande atajwe.Tufafanuliwe vizuri kuhusu afande aliyetajwa.ALAFU WAVUTA BANGI TUSIVUNJIWE HESHIMA KWANI NI WASTAARABU KUSHINDA WACHACHE KWENYE GESHI LA WAUAJI WA KUDUNGA SINDANO ZA SUMU KULE MTWARA.
Hivi ile kesi iliishiaje au ndio ilifunikwa kombe na Mwanaharamu akapita.
 


Ameandika Dkt. Gwajima D katika Mtandao wa X.

Ndugu Wananchi, nimepokea 'Tags' nyingi za maoni na maswali kuhusu taarifa iliyotolewa na RPC mkoa wa Dodoma juu ya mwenendo wa shauri la 'Binti wa Yombo' (reja taarifa za awali).

Ndugu Wananchi, nimepokea hisia zenu, maoni na maswali yenu ambayo mmeelekeza kwangu. Nimewasiliana na Mhe Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye tayari naye amepokea na anafanyia kazi hivyo, tumpe nafasi atatoa taarifa yake.

Ndugu Wananchi, ni dhahiri kuwa, alichofanyiwa 'Binti wa Yombo' ni kitu kibaya kisicho cha utu hivyo, anastahili haki yake kwa mapana yote.

Ndugu Wananchi, Nawasihi tujipe muda na kuamini kuwa, haki itatendeka kwa mujibu wa sheria na itaonekana bayana na siyo vinginevyo.

Pia soma: Polisi: Wanaotuhumiwa kubaka na kulawiti ni kama wavuta bangi, hawakutumwa na Afande, yule dada alikuwa kama anajiuza

View attachment 3073878
Kwa hiyo usipofuatilia ndio haki inapotea hivyo? Hii siyo sawa kama kuna taasisi wanapokea mshahara kupindisha sheria. Na rais na wengine wapo. Tuseme hapana kwenye hili
 
Matukio yanayojulikana mitandaoni ni machache kulinganisha na ambayo hayajulikani, mfumo wa jeshi mbovu sana na haki za watu zitaendelea kupotea kama tutaishi kwa kutegenea matamko ya wanasiasa, mpaka jamii itumie nguvu kubwa mtandaoni ndipo waziri aongee na waziri mwenzie kuchukua hatua, ni kama kuficha uchafu chini ya uvungu, nchi, serikali, jeshi vyote ni uozo kuna binti miaka 7 kalawitiwa na kubakwq lakini huwezi amini polisi buguruni walianza kuwashutumu wazazi husika wa binti,, chura kiziwi hizi laana unazitafuta kwa nguvu sana
 
Unisamehe bure mama Dr Gwajima. Sijawahi kukulaumu hata siku moja. In fact mimi ni shabiki lia lia wako, muda mfupi uliopita Nime- react hapa kwenye post ya mtu kuwa mara hii kwa mara ya kwanza uko kimya. Kumbe nime ku- Pre empty. Samahani ma'am. Grace and Mercy shall speak for you.
 
Hata kufanya uchafu huo Kwa kuridhia ni kosa
Tusubiri mamlaka za kiuchunguzi zije na majibu yanayoeleweka tusihukumu Kwa hisia
Hawa mabinti nao sio wa kuaminika sana.
Binafsi nasubiria police watupe uthibitisho me Sina uhakika na lolote
Kwahiyo hata video ile haikupi uhakika wowote!? Kwamba hujaona kuwa binti alifanyiwa kitendo kichafu bila ridhaa yake!? Upande uliochagua ni mgumu sana na huwezi kuutetea, pole sana.
 
Kwahiyo hata video ile haikupi uhakika wowote!? Kwamba hujaona kuwa binti alifanyiwa kitendo kichafu bila ridhaa yake!? Upande uliochagua ni mgumu sana na huwezi kuutetea, pole sana.
Nimekwambia subiri mahakama
Me sijahukumu chochote
Nitaiamini mahakama tu
 
Acha hisia police wanafanya uchunguzi wewe unawapinga bila utafiti wowote
Peleka ushahidi kama alibakwa.
Hivi mtu abakwe na wanaume 4 akae kimya Toka mwezi wa 4
Haya alitibiwa wapi hayo majeraha ya kubakwa? Bila pf3
Kwa hiyo wewe kuhusu kubakwa athari yake umetafsiri kuwa ni majeraha tu?
Vipi kuhusu psychology?
 
Mdogo wangu nilimnyima pesa ya kuprint vyeti wakati anataka kuomba kazi na sikumpa ushirikiano kabisa.

Sikumwambia kwanini nilimzungusha mpaka dead line ikaisha.

Nikakausha.
Hongera sana mkuu kwa ulichokifanya. Tunatakiwa tuwe na watu 100 wengine kama wewe.
Yupo mtoto wa shangazi ni police tumesoma nae kuanzia la kwanza hadi kidato cha nne akapata nafasi ya kwenda police.

Tangu aajiriwe tu udungu uliishia hapo na hata akija huwa sitakagi nimuone kabisa
hajawahi nikosea wala kumkosea lkn hii kutokumpenda kulianzia alipo ajiriwa tu.


hata tukikutana msibani nk bado kabisa nakuwa mbali sana nae.
kwakweli police hata akiwa mwanangu nahesabu nimepoteza bora ningepiga nyeto wala hela yake siwezi omba.

laana hizi
 
Kwa hiyo waziri wa mambo ya ndani yeye haoni wala kusikia MPAKA UMKUNBUSHE
acheni kuwa mnatuona mazwazwa
hili jambo linachafua na kuondoa imani kwa polisi,na pia kwa viongozi wote wanawake kama hamuwezi hata kutetea haki ya mmoja wenu
Mnatuaminisha munaweza kutete masilahi ya TAIFA,
Wako wapi wale viongozi wa wanawake wa chadema,ccm,Act pamoja na
UWT
lIko wapi baraza la waandishi habari wanawake,madakitari wanawake
KIMSINGI JUMUIYA ZOTE ZENYE MASILAHI NA WANAWAKE ZIMEFELI
 
Back
Top Bottom