A
Anonymous
Guest
Kwa kipindi cha hivi karibuni, kuna jambo ambalo limeendelea kunishangaza. Katika nyakati tofauti, nimeshuhudia watoto walio chini ya umri wa miaka 15 wakifanyishwa kazi ya kuzungusha na kuuza mayai ya kuchemsha katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Baadhi ya watoto hao niliofanikiwa kuzungumza nao walinieleza kuhusu umri wao na mazingira wanayoishi. Kwa mujibu wa maelezo yao, wengi wanadaiwa kuletwa kutoka mikoani na watu mbalimbali ili kufanya shughuli hiyo.
Pia soma ~ Olengurumwa: Watoto wanaopelekwa mijini kuuza mayai na kazi nyingine wananyimwa Haki ya Elimu
Jambo la kushtua zaidi ni kwamba watoto hao hukaa mitaani hadi nyakati za usiku. Kwa mfano, mara kadhaa nikiwa katika baa zilizopo eneo la Makonde, Mbezi Beach, nimeshuhudia watoto hao wakipita maeneo hayo hadi majira ya saa tatu usiku wakitafuta wateja.
Huenda jambo hili likaonekana la kawaida kwa baadhi ya watu, lakini ukweli ni kwamba usalama wa watoto hao uko hatarini. Aidha, wananyimwa haki zao nyingine za msingi, ikiwemo haki ya kupata elimu, malezi bora na kukua katika mazingira salama.
Natoa wito kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, kupitia kwa Waziri Dorothy Gwajima, kuchukua hatua za haraka kuchunguza na kukomesha tabia ya watu wanaowatoa watoto vijijini na kuwapeleka mijini kufanya kazi zinazokiuka sheria, taratibu na haki za watoto.