DOKEZO Responded Waziri Gwajima, fuatilia wimbi la watoto wanaofanyishwa biashara ya kuuza mayai mitaani hadi usiku

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kwa kipindi cha hivi karibuni, kuna jambo ambalo limeendelea kunishangaza. Katika nyakati tofauti, nimeshuhudia watoto walio chini ya umri wa miaka 15 wakifanyishwa kazi ya kuzungusha na kuuza mayai ya kuchemsha katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Baadhi ya watoto hao niliofanikiwa kuzungumza nao walinieleza kuhusu umri wao na mazingira wanayoishi. Kwa mujibu wa maelezo yao, wengi wanadaiwa kuletwa kutoka mikoani na watu mbalimbali ili kufanya shughuli hiyo.

Pia soma ~ Olengurumwa: Watoto wanaopelekwa mijini kuuza mayai na kazi nyingine wananyimwa Haki ya Elimu

Jambo la kushtua zaidi ni kwamba watoto hao hukaa mitaani hadi nyakati za usiku. Kwa mfano, mara kadhaa nikiwa katika baa zilizopo eneo la Makonde, Mbezi Beach, nimeshuhudia watoto hao wakipita maeneo hayo hadi majira ya saa tatu usiku wakitafuta wateja.

Huenda jambo hili likaonekana la kawaida kwa baadhi ya watu, lakini ukweli ni kwamba usalama wa watoto hao uko hatarini. Aidha, wananyimwa haki zao nyingine za msingi, ikiwemo haki ya kupata elimu, malezi bora na kukua katika mazingira salama.

Natoa wito kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, kupitia kwa Waziri Dorothy Gwajima, kuchukua hatua za haraka kuchunguza na kukomesha tabia ya watu wanaowatoa watoto vijijini na kuwapeleka mijini kufanya kazi zinazokiuka sheria, taratibu na haki za watoto.
 
Shida tupo bize kukemea matokeo na sio chanzo. Hao watoto kuwa mitaani wakiuza mayai ni matokeo ya process iliyokamilika ambayo imezalisha kinachoonekana mtaani.

Kimsingi tudeal na chanzo,watu kukatikiana viuno bila utaratibu mzuri wa kuwaandalia watoto kaya za kuishi na kuweza kuita nyumbani na kuishi kwa utulivu.
 
Wanaanza kutembeza saa 4 asubuhi hadi saa 4 usiku pia nawaonaga. Hawa vijana ni kuanzia 12 hadi 16. Wanatembea umbali mrefu, umbali mrefu sana kwa siku na sidhani kama wana lishe nzuri na malazi mazuri.

Wengi wao ni kutoka Kigoma/Waha na huko mikoa ya Mara sijui Tarime na kidogo Mwanza na Dodoma.
 
Watu zaeni kutokana na huwezo wenu wakuhudumia na si kufyatua tu..
 
Mimi ndio maana napiga sana kelele kwa maskini choka mbaya wanaozaliana kama mapanya. Wanaleta watoto duniani kuja kuteseka bure.

Kungekuwa na uwezekano wa kuzuia mtu asizae. Maskini, mafukara na wajinga wote ninge fanya wasizae.

Mtu maskini akizaa mtoto anaongeza maskini mwingine duniani.
 
Inasikitisha sana aisee.
 
Unakumbuka juzi juzi kulikuwa na kichaa mmoja alikuwa anawahimiza wananchi wazae kwa wingi kama wanafyatua? Na viongozi wenzake wanacheka na kushangilia kama amesema jambo la maana? Kipindi cha mwalimu kulikuwa na kitu kinachoitwa UMATI. Chama cha kushauri watu kuhusu uzazi wa mpango. Sera ya uzazi Tanzania imefeli sana sana na kuja kuiweka sawa sasa hivi itachukuwa miaka zaidi ya 50.
 
Inabidi sasa itungwe sheria kali kwa wanaotelekeza watoto wao.
Tatizo siyo sheria bali tatizo ni kuwa kila kitu kuhusu uongozi kime-collapse. Nchiinajiendea bora liende, wenyewe wako busy kufanya ufisadi na starehe huku wakiwekeza nguvu kubwa kwenye kuwinda wakosoaji.
 
Kabisa mkuu.
 
Serikali itoe agizo kwa yeyote anaye tumikisha mtoto akamatwe na kufunguliwa mashitaka
Jamii pia ikemee na kupinga ajira kwa watoto naamini itasaidia
 
Family planning imeshindikana kote afrika ya mtu mweusi (sub saharan) hakuna hata nchi moja iliyotoboa. India yenyewe nayo imeshindwa, mana watoto wengi na umaskini havitenganagi pakubwa. The more the poor the higher fertility
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…