Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Mhe. Waziri mama Dkt. Gwajima D hongera kwa majukumu.
Hoja yangu ni fupi.
Katika vibanda vya kusubiria abiria wanaotumia vivuko pale Kivukoni na Kigamboni kuna Watanzania wenzetu walioamua kuwa ombaomba ili wapate pesa za kujikimu.
Pamoja na kwamba wanaomba pale kwa muda mrefu, lakini sasa wameonekana kuwatumia watoto wadogo kwenye shughuli hiyo. Jambo hilo tunaliona maeneo mbalimbali nchini
Hoja yangu ni kuhusu Haki ya Mtoto hususani kwenye malezi na elimu. Je, watoto wale wanalindwaje na jamhuri waweze kupata elimu na hata malezi kama watoto wengine?
Nafahamu ombaomba fulani pale Moroco mataa ambapo hapo zamani alikuwa mtoto anaongozana na baba yake wakiomba eneo hilo.
Ahsante