Waziri Gwajima: Majukwaa kama JamiiForums.com yanaibua Sauti za Wananchi na kuongeza uwajibikaji

Waziri Gwajima: Majukwaa kama JamiiForums.com yanaibua Sauti za Wananchi na kuongeza uwajibikaji

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalumu, Dorothy Gwajima akizungumza mara baada ya kupewa tuzo na JamiiForums kwa kuwa kiongozi anayepokea maoni ya Wananchi na kuyafanyia kazi amesema kuwa majukwaa ya Kidigitali yanasaidia kuongeza uwajibikaji sambamba na kuisongeza zaidi Serikali kwa Wananchi.

"Tuzo hizi kwangu mimi zinanipa hasa hali zaidi, kasi zaidi ya kuendelea kusikiliza sauti za Wananchi na hiki ni kielelezo cha ulimwengu wa kidigtali ambayo imekuja nyakati zetu kuwa msaada mwema kwa Serikali ambayo lengo lake ni kuwahudumia Wananchi"amesema Waziri Gwajima

Anaongeza "Kwahiyo kama kiongozi wa Serikali napongeza sana kwa sababu wananchi sasa hivi wanaweza wakawa katika maeneo ambayo sauti yao haiwezi kusikika au katika maeneo ambayo baadhi ya waliopewa majukumu na Serikali wawatumikie wananchi wako na wengine wasiowajibika lakini wapo na wengine wanaowajibika vizuri lakini hatuwasikii kwa urahisi huku. Kwahiyo ni pande mbili inaibua sauti ya wananchi kwenye kutoa maoni yao kwa Serikali yao , kwenye kumpongeza wanaopongezwa na wanaolalamikiwa pia wanaibuliwa."

Amesema kuwa Viongozi wa Serikali ambao wamepewa dhamana wanatakiwa kufurahia na kuwa tayari kupokea masuala mbalimbali ambayo yamekuwa yakiwasilishwa na Wananchi kisha kuyatolea mrejesho kwa uharaka.

"Kwetu sisi kama Serikali tunatakiwa tufurahi, tunatakiwa tupokee na tutoe mrejesho kwa wananchi haraka sana, kwa kufanya hivyo ndivyo tunaisogeza Serikali mikononi mwa wananchi wao wenyewe lakini inaongeza uwajibikaji. Mtu anakuwa anaona kwamba kumbe macho ya Serikali yapo nilipo kwa msaada wa majukwa haya, kwahiyo kama hataki kuwajibika atawajibika tu ndio Dunia ambayo sasahivi tunaishi," amesema Waziri Gwajima.

Itakumbukwa JamiiForums ilitoa tuzo kwa kiongozi huyo pamoja na mamlaka mbalimbali za kiserikali ambazo zimekuwa mstari wa mbele kutoa taarifa na mrejesho wa masuala mbalimbali ambayo yamekuwa yakiibuliwa na wadau ndani ya jukwaa la JamiiForums. com, sambamba na tuzo hizo pia ilitoa tuzo kwa washindi wa shindano la StoriesofChange.
 
Back
Top Bottom