A
Anonymous
Guest
Hivi karibuni nimeshuhudia kitendo kikubwa sana cha unyanyasaji, udhalilishaji na ukatili aliofanyiwa Mwanamke mmoja jirani na kwangu dhidi ya mwenye nyumba wake, nikaona si vyema kulikalia kimya tukio hili ni lazima nilitolee taarifa ili wahusika wamsaidie mwanamke huyo na jamii ijifunze.
Majira ya saa mbili za usiku siku ya Alhamisi tarehe 17. 10.2024 nilisikia sauti ya baba mwenye nyumba huyo akisema kesho muondoke siwataki hapa.
Na wewe Mwanamke kesho mumewe akitoka asubuhi kwenda ofisini ufuatane naye huko huko ukikuacha hapa utakiona cha moto nitakufanya kitu kibaya (kwa sauti ya ukali sana akaingia ndani kwake akafunga mlango paaaa)!
Ikanibidi asubuhi nimuulize yule Mwanamke kulikoni mbona jana mwenye nyumba alikuwa anazungumza kwa sauti ya ukali sana shida hasa ni nini.
Akasema aliwaambia mwisho wa mwezi huu wasitishe mkataba, na mume wake yupo kwenye mchakato wa kutafuta nyumba nyingine kabla ya mwisho wa mwezi.
Akanieleza kuwa tayari walisha kubaliana ila anashangaa anapitia vitisho na manyanyaso kwa kitu ambacho walishazungumza wao wenyewe kama wanaume.
Hata asubuhi ya leo baada ya mume wake kwenda ofisini alienda kugonga mlango wake kwa nguvu sana akimuulizia mume wake ili hali alimuona katoka asubuhi na mapema kuelekea kazini.
Akanieleza kwa baaada ya kufungua mlango akamfokea sana na kusema nataka muondoke sitaki kuwaona na maneno mengine yasiyo ya kistaarabu kwa sauti ya juu na ukali sana.
Mwanamke huyo anasema kinachomtisha zaidi ni kwamba kwanini anashambuliwa huyo mwenye nyumba anamsumbua yeye pindi tu mme wake akiondoka mbona mume wake akiwepo hafanyi hivyo.
Nimerudi jioni kutoka mizunguko yangu siku ya ijumaa usiku sikumkuta yule dada baadae nikampigia simu akasema ameondoka amenda kukaa kwa dada yake maana roho yake haina amani kwa vitendo na maswahibu kutoka kwa mwenye nyumba.
Nikamuuliza vipi kuhusu biashara yako ya maandazi itakuwaje na wateja wameanza kuongezeka,akasema anahitaji kwanza kutulia apate amani ya moyo maana vitisho vikali vilimuathiri hakuwa na amani hata kidogo na ameshamwambia mume wake waamie mahali pengine yeye hawezi kuishi tena pale.
Nikajaribu kumshauri aende kufungua kesi dhidi ya unyanyasaji, udhalilishaji na ukatili aliotendewa maana ni haki yake ya kisheria.
Akasema anaogopa hajawahi kwenda polisi wala mahakamani kwa hiyo hawezi kufanya hivyo yeye anamuachia Mungu tu.
Nimejaribu sana kumshawishi amekataa ila leo nataka niongee na mume wake azungumze naye ili tuweze kwenda kutafuta haki yake ya kisheria dhidi ya unyanyasaji na udhalilishaji huo.
Hata kama nyumba ni yake ila asiitumie kwa ajili ya kunyanyasa na kuumiza wengine maana hata mpangaji nae ana haki zake.
Katika hili tunaomba Mh waziri na vyombo vinavyohusika kumsaidia mwanamke huyu dhidi ya unyanyasaji wa kiwango hiki kisicho vumilika mpaka mtu anakimbia nyumba anayoishi.
Mimi nipo tayari kutoa ushirikiano katika hili.
~SAIDIENI JAMII