DOKEZO Waziri Gwajima, mwanamke huyu anafanyiwa ukatili na unyanyasaji kutoka kwa baba mwenye nyumba wake

DOKEZO Waziri Gwajima, mwanamke huyu anafanyiwa ukatili na unyanyasaji kutoka kwa baba mwenye nyumba wake

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hapo hakuna unyanyasaji, ni wivu wa mapenzi na tamaa za ngono ndio zmetawala
cha msingi wahame tu hapo, wakapange kwingine

alafu kesi kama hizo mwenyekiti wa mtaa anaweza kutatua sio mpaka umsumbue waziri
huyo baba mwenye nyumba aelewe kwamba kisheria mpangaji anapewa notice mwezi mmoja ndio mpangaji ana hama, tena mwezi huo anatakiwa akae bure

huyo dada ni pisikal naona wewe na baba mwenyenyumba mnawekea bifu kisa mke wa mtu
 
Mtoto wa kiume mbea kama Kitu gani!...
Una mpaka number ya simu hali huyo mwanamke ana aidha mume au njemba yake ....

Hivi nyinyi GEN-Z mnakwama wapi?
Halafu anaweza kumpigia mkewe, lakini mmewe mpaka ameandika hapa hajampigia wala kumuita amshauri!!!
Inawezekana mwenye nyumba kanyanyaswa, na hizo ni reaction baada ya kufanyiwa strange actions.

Kodi wamelipa kama walivyokubaliana? Yani anataka waziri aingilie jambo ambalo majirani na wajumbe, serikali ya mtaa/kijiji kinaweza kufanyia kazi!!!
 
Mara nyingine maisha lazima yawe rafu ili yawe na maana..yani mnataka sasa watu wasigombe hata kidogo jamani..labda alimlia hela zake akamwambia atamrejeshea? Labda ameamua kumgombeza mumewe akiwa hayupo ili asimchafulie CV kwa mumewe...
Mambo mengine muwe mnaangalia na kuyaacha...ukatili ni kipigo cha mbwa koko mpk kukata viungo...labda..ubakaji...ulawiti...
 
Wewe kama kweli unapenda kusaidia na mapambano, kachonganishe serikali ya mtaa, kalalamike kuwa jamaa katoa lugha chafu hadharani na vitisho, ambayo ni kinyume kwa mujibu wa sheria ya nchi, na adhabu yake ni kifungo cha mpaka miezi sita.

Omba aitwe 😆 , mengine yataendelea huko
 
Mi nilichoelewa ni kwamba wewe na mwenye nyumba mnamtaka huyo mwanamke. Ila kesho ntasoma vizuri ntakuja na maoni tofauti
 
Dahhh....
Hii nchi bhana...😟
Yaani hili nalo hadi aje alisimamie waziri..☹️
Yaani jambo la mume kusimama asubihi na kumwambia mwenyenyumba "siku nikikuta umemfikea mke wangu utanitambua"
Hivi wanaume wahuo mkoa mbona mnakua wanyonge hadi kwenye mambo madogo ya kumaliza nyie wenyewe..🤔
Hili mbona hata maafisa jamii wa ofisi za watendaji wa kata wanalimudu na kulimaliza kabisa...😶
 
Na wewe unavizia mme atoke na mwenye nyumba hivyo hivyo.

Atakuwa anasumbua kulipa kodi.

Hayo siyo ya kumwambia Mheshimiwa.
 
Mnataka kumchosha tu mama mkwe wangu gwajima na petty issue na kuacha mambo ya msingi.kufokewa tu unataka aende mahakamani?
 
Hivi karibuni nimeshuhudia kitendo kikubwa sana cha unyanyasaji, udhalilishaji na ukatili aliofanyiwa Mwanamke mmoja jirani na kwangu dhidi ya mwenye nyumba wake, nikaona si vyema kulikalia kimya tukio hili ni lazima nilitolee taarifa ili wahusika wamsaidie mwanamke huyo na jamii ijifunze.

Majira ya saa mbili za usiku siku ya Alhamisi tarehe 17. 10.2024 nilisikia sauti ya baba mwenye nyumba huyo akisema kesho muondoke siwataki hapa.

Na wewe Mwanamke kesho mumewe akitoka asubuhi kwenda ofisini ufuatane naye huko huko ukikuacha hapa utakiona cha moto nitakufanya kitu kibaya (kwa sauti ya ukali sana akaingia ndani kwake akafunga mlango paaaa)!

Ikanibidi asubuhi nimuulize yule Mwanamke kulikoni mbona jana mwenye nyumba alikuwa anazungumza kwa sauti ya ukali sana shida hasa ni nini.

Akasema aliwaambia mwisho wa mwezi huu wasitishe mkataba, na mume wake yupo kwenye mchakato wa kutafuta nyumba nyingine kabla ya mwisho wa mwezi.

Akanieleza kuwa tayari walisha kubaliana ila anashangaa anapitia vitisho na manyanyaso kwa kitu ambacho walishazungumza wao wenyewe kama wanaume.

Hata asubuhi ya leo baada ya mume wake kwenda ofisini alienda kugonga mlango wake kwa nguvu sana akimuulizia mume wake ili hali alimuona katoka asubuhi na mapema kuelekea kazini.

Akanieleza kwa baaada ya kufungua mlango akamfokea sana na kusema nataka muondoke sitaki kuwaona na maneno mengine yasiyo ya kistaarabu kwa sauti ya juu na ukali sana.

Mwanamke huyo anasema kinachomtisha zaidi ni kwamba kwanini anashambuliwa huyo mwenye nyumba anamsumbua yeye pindi tu mme wake akiondoka mbona mume wake akiwepo hafanyi hivyo.

Nimerudi jioni kutoka mizunguko yangu siku ya ijumaa usiku sikumkuta yule dada baadae nikampigia simu akasema ameondoka amenda kukaa kwa dada yake maana roho yake haina amani kwa vitendo na maswahibu kutoka kwa mwenye nyumba.

Nikamuuliza vipi kuhusu biashara yako ya maandazi itakuwaje na wateja wameanza kuongezeka,akasema anahitaji kwanza kutulia apate amani ya moyo maana vitisho vikali vilimuathiri hakuwa na amani hata kidogo na ameshamwambia mume wake waamie mahali pengine yeye hawezi kuishi tena pale.

Nikajaribu kumshauri aende kufungua kesi dhidi ya unyanyasaji, udhalilishaji na ukatili aliotendewa maana ni haki yake ya kisheria.

Akasema anaogopa hajawahi kwenda polisi wala mahakamani kwa hiyo hawezi kufanya hivyo yeye anamuachia Mungu tu.

Nimejaribu sana kumshawishi amekataa ila leo nataka niongee na mume wake azungumze naye ili tuweze kwenda kutafuta haki yake ya kisheria dhidi ya unyanyasaji na udhalilishaji huo.

Hata kama nyumba ni yake ila asiitumie kwa ajili ya kunyanyasa na kuumiza wengine maana hata mpangaji nae ana haki zake.

Katika hili tunaomba Mh waziri na vyombo vinavyohusika kumsaidia mwanamke huyu dhidi ya unyanyasaji wa kiwango hiki kisicho vumilika mpaka mtu anakimbia nyumba anayoishi.

Mimi nipo tayari kutoa ushirikiano katika hili.

~SAIDIENI JAMII
Hebu tuanzie hapa, "maana hata mpangaji nae ana haki zake", haudhani haki ya mpangaji inaanzia anapolipa kodi kwa wakati! Haudhani mwenye nyumba kodi ya jengo na ardhi huanzia anapozilipa kwa wakati! Nini kitatokea asipozilipa kwa wakati hizo kodi za serikali? Je, huwa zinamajadiliano kati ya serikali na mwenye nyumba? Au wao wakija hupiga mnada nyumba?
Unamuuliza kuhusu biashara yake ya maandazi inavyoshamiri huku ukishindwa kumuuliza kwanini pesa anazopata wasilipe kodi! Ni vipi unavyoweza kumpigia simu mke wa mtu kama hauna maslahi naye huku ukishindwa kuongea na mme wake? Hapa kuna namna na unajaribu kutetea maslahi yako.
Mwisho, unajua kuna watu wanaishi kwa kuhamahama vyumba bila kulipa kodi! Huishi kwa miezi mitatumitatu anahama bila kulipa kodi.
Ukimpeleka unakodhani atapata haki atapewa haki yake ya kulipa kodi, utajuta.
 
Itoshe tu,kusema mtoa mada unajambo lingine tofauti na,hili ulilolileta,apa jukwaani na,unahisi unao,wasimulia wanaweza kuwa na,akili kama,zako upuuzi mwingine muwe,mna,uacha uko,uko,Fcbk.
 
Watu wajinga wajinga kama nyie ndio mtafanya watu wenye shida genuine washindwe kusaidika
 
Back
Top Bottom