Waziri wa afya Dr Gwajima ameupongeza mkoa wa Mbeya kwa ujenzi wa jengo la kisasa la wajawazito.
Dr Gwajima amesema LEO amefurahi sana.
Waziri wa afya yuko ziarani mkoani Mbeya akikagua shughuli mbalimbali za wizara yake.
Source Upendo tv
Maendeleo hayana vyama!
Huyo mama nimemwondoa kabisa katika watu wa maana nchi hii. Aheri kumsikiliza Musukuma kuliko huyu mama.
Daktari mzima anaendekeza mambo ya nyungu, ujinga ambao hauna uthibitisho wa kisayansi, tena kwa nadharia ya kisayansi (nyungu) inaongezea tatizo la mgonjwa wa covid kujaa mapafu maji.
Siku huyu mama akiugua covid asipewe tiba yoyote, apelekwe kwenye nyungu.
Daktari mzima anaacha taaluma na kushabikia tiba za wale waganga washirikina wa usukumani wanaofuga fisi, eti ndiyo vyombo vya usafiri na viumbe vya kuwaletea nyama nyumbani.
Wanataka kuligeuza Taifa zima liache tiba za kisayansi, wageukie ushirikina.
Nadhani leo mmemsikia DC wa Nyang'wale akielezea shida kubwa ya fisi wanaofugwa na wasukuma kishirikina wanavyotishia mifugo na binadamu, na eti sasa wameomba timu ya wataalam wa jadi (maana yake wenye uchawi zaidi) toka Shinyanga, na kwamba kwa msaada wao, tayari wameua fisi 28. Huko ndiko usukumani ambako Gwajima anataka Watanzania wote watumie hizo tiba za kishirikina kutoka kwenye mazingira aliyokulia.