JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amewataka baadhi ya wanaume ambao bado wana mfumo dume wa kunyanyasa wanawake kuacha tabia hiyo hasa kwenye masuala ya uchumi.
Dkt. Gwajima ameyasema hayo mjini Morogoro Wakati akizungumza kwenye Kongamano ambalo limewakutanisha wanawake Zaidi ya 150 kutoka katika mikoa tofati ambalo liliandaliwa na taasisi binafsi inayoitwa Ladies Talk.
Dkt. Gwajima amesema kumekuwa na ongezeko la wajane nchini kwa sababu wanaume wanapoteza maisha kuliko wanaume huku akieleza kuwa baadhi ya sababu hizo ni vifo vinavyotokana na wivu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa taaisisi hiyo ya Ladies Talk Salome Sengo amesema lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wanawake pamoja ili waweze kutangaza biashara zao ikiwa ni pamoja na kupata elimu ya ujasiriamali.