#COVID19 Waziri Gwajima: Watu 7 kati ya watu 10 wanaokufa kwa Corona wanakuwa hawajachanjwa 3 tu ndio wamechanjwa!

#COVID19 Waziri Gwajima: Watu 7 kati ya watu 10 wanaokufa kwa Corona wanakuwa hawajachanjwa 3 tu ndio wamechanjwa!

Waziri muongo. Maana yake anataka kusema 30% ya watanzania wamechanja???? Yaani watanzania milioni 15 wamechanja??? Mungu tusaidie na huu uongo uishe basi ili tuijenge nchi

Wapi kasema 30% wamechanjwa?

Waziri kasema katika wanaokufa kwa korona 30% ndiyo walikuwa wamechanjwa.

Kipi hutaki kuelewa hapo?
 
Na katika hao 10 wanaokufa ni wangapi wanakuwa wamepiga nyungu, wametafuna vitunguu na kujifukizisha ?View attachment 2053927View attachment 2053928View attachment 2053929View attachment 2053930

IMG-20210725-WA0007.jpg

IMG_20210806_053407_437.jpg
 
Aseme pia ktk 10 ambao wamepona, wangapi hawajachanjwa.

Je katika kumi wanaopona ambao wamechanjwa hao hamwataki?

Nyie watu vipi?

70% ya watu wanaokufa hawakuchanjwa haiwafikirishi bali mmetanguliza ujuaji tu?

Wanaokufa kwa takwimu hizi wangeweza kuokolewa maisha yao kwa chanjo tu.
 
Watu wangapi wamechanjwa mpaka sasa hapa Tanzania?
Hizi asilimia za wanaokufa zinapatikana vipi Kwa waliochanja na wasiochanja.
 
Mama atangaze haraka hiyo wizara mpya na waziri wake, kuchelewesha kutazidi kumdhalilisha huyu waziri. Hii yote ni kutaka kusikika tu kwamba yupo.
 
Waziri wa afya Dr Gwajima amesema katika watu 10 wanaokufa kwa ugonjwa wa Corona 7 wanakuwa hawajachanjwa na 3 tu ndio waliochanjwa.

Utafiti unaonyesha hata hao watatu waliochanjwa hufariki kwa sababu huwa na magonjwa mengine nyemelezi.

Source: ITV habari
Huo uchambuzi na hitimisho (conclusion) hauko scientific kimaheHizo takwimu hazijafanyiwa mlinganisho wa kisayansi. Zingalikuwa na kaukweli kama nusu ya watanzania wangalikuwa wamechanja na nusu hawajachanja. Yaani kama uwiano (ratio ingalikuwa 1:1.

Sasa hali halisi ni kwamba kati ya watanzania milioni 60 ni millioni 1 tu ndiyo waliochanja. Hivyo ratio ni 60:1. Hii maana yake ni kuwa kama ngoma ingalikuwa draw kati ya wasiochanjwa na waliochanjwa (ie chanjo hazina effect ya kupunguza vifo) ratio ingalikuwa vifo 60:1 au 180:3. Sasa hii 7:3 maana yake ni kuwa waliokufa wakiwa wamechanja ni wengi zaidi kuliko wale waliokufa bila kuchanja. Hizi ni hesabu tu za uwiano. You need a controlled study.
 
Watu wangapi wamechanjwa mpaka sasa hapa Tanzania?
Hizi asilimia za wanaokufa zinapatikana vipi Kwa waliochanja na wasiochanja.

Watakuwa wangapi wamechanjwa hilo ni jambo jingine.

Asilimia za wanaokufa zinaptikana hivi:

1. Angalia katika jumla ya watu waliokufa kwa Corona.
2. Kutokea hapo #1 katika hao wangapi kwa wastani walikuwa wamechanjwa na wangapi kwa wastani walikuwa hawakuwa wamechanjwa.

Mfano kama jumla ya wafu ilikuwa ni 40,
kwamba katika hao waliokuwa hawakuchanjwa ni 28, na waliokuwa wamechanjwa ni 12 basi:

Kwa wastani kumbe katika 10, wasiochanjwa ni 7 na waliochanjwa ni 3.

Unachagua kufa kundi lipi hapo mjomba?
 
Huo uchambuzi na hitimisho (conclusion) hauko scientific kimaheHizo takwimu hazijafanyiwa mlinganisho wa kisayansi. Zingalikuwa na kaukweli kama nusu ya watanzania wangalikuwa wamechanja na nusu hawajachanja. Yaani kama uwiano (ratio ingalikuwa 1:1.

Sasa hali halisi ni kwamba kati ya watanzania milioni 60 ni millioni 1 tu ndiyo waliochanja. Hivyo ratio ni 60:1. Hii maana yake ni kuwa kama ngoma ingalikuwa draw kati ya wasiochanjwa na waliochanjwa (ie chanjo hazina effect ya kupunguza vifo) ratio ingalikuwa vifo 60:1 au 180:3. Sasa hii 7:3 maana yake ni kuwa waliokufa wakiwa wamechanja ni wengi zaidi kuliko wale waliokufa bila kuchanja. Hizi ni hesabu tu za uwiano. You need a controlled study.

Sayansi inakuja vipi wakati hamuitaki?

IMG_20211211_082805_567.jpg
 
Kwani huyo udaktari wake (PhD) ni wa sayansi kama wa kwangu?

Kwa vile umemkana huyo mwamba ninarejea kuangalia bandiko lako.

Waziri kasema chukua idadi yote ya wagonjwa waliokufa kwa korona katika kipindi chochote sasa. Utaona:

70% yao hawakuwa wamechanjwa.
30% yao walikuwa pia wamechanjwa.

Tatizo liko wapi hapo kiasi cha kutoa povu na doctorate yako?
 
Nadhani maelezo ya huyo mwafrika hayako inline na ya Dr Fauci. Mtu aliekuwa vaccinated (aliechanjwa) anaweza kutransmit corona na anaweza pia kuwa mgonjwa, tofauti yake iko kwenye critical levels zao ni tofauti.

Aliekuwa unvacinated yuko kiufupi hatarini au kupata corona na kuwa mgonjwa wa kulazwa hospitali na mitungi ya oxygen, wakati aliekuwa vacinated akawa na kijihoma kidogo na kuendelea na shughuli zake siku mbili tatu baadae.

Kitu kimoja ambacho ni fact, suala hili linadeal na virus. Nadhani hakuna njia ya kuwa na kinga ya 100%, ukipiga dozi 2 anaibuka omicron unaambiwa uongeze dozi. Worst case inaweza kuja version/variant ambayo vacine haijacover completely.

Kwa wanaofahamu hili suala la virus na vaccine sio jipya katika jamii na dunia kwa ujumla.
 
Dawa za Ukimwi mnabugia kila siku hamuogopi lakini chanjo za corona ndiyo mnaziogopa? Chanjeni ili msije mkatengeneza variant mpya na sisi tukapigwa travel ban kama wenzetu wa Afrika Kusini. Nyerere angekuwa hai angewatukana sana nyie mnaopinga chanjo.
 
Back
Top Bottom