Waziri Hussein Bashe nifikishie pongezi hizi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu bei ya korosho

Waziri Hussein Bashe nifikishie pongezi hizi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu bei ya korosho

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Kwanza nakusalimia sana Mhe Waziri wa Kilimo.

Nina mengi sana ya kusema lkn sitak nikuchoshe.

Kubwa zaidi nataka nikwambie kuwa leo Jumapili Wakulima wa korosho Lindi wameuza korosho zao kilo kwa efu 4150 kule Ruangwa na 4025 kule Nachingwea.

Wananchi wa mkoa huo wamefurahia mno korosho kuwa na soko zuri.

Waziri Bashe nimewasikia ndugu zangu wakisema mara ya mwisho watu wa Kusini kufurahia bei ya zao hilo ni mwaka 2019 wakati Rais Magufuli alipozinunua korosho zote.

Wananchi hata kwenda kujiandikisha wanaona shida tu maana kila mtu ananuka hela.

Ziara za Mhe Rais nje ya nchi zina manufaa makubwa na moja ya manufaa yake ndio haya sasa.

Mhe Bashe mfumo wa TMX hauna longo longo kaka, mambo yote ni online trading system na kila mtu anaona

Mwambie Dkt Samia Suluhu Hassan wananchi wa Mtwara na Lindi tunamuombea kwa mungu afya njema aendelee kutuletea neema.

Ombi langu wakulima wapewe elimu kwa sababu nchi zinazolima korosho duniani ziko 46 na kwa vile nchi nyingine hazijaanza msimu bado basi wakulima wakimbizane na minada ili kuwahi soko maana akina Cambodia, Ivory Coast Cameron india Nigeria vietnam wakianza tu huku tumekwisha.

Aidha naomba wakulima waelimishwe kupitia Wakuu wa Wilaya, ma das, ma ded maafisa Kilimo kata, matarafa nk kuwaelimisha wakulima kupeleka korosho safi ghalani ili wasiharibu soko

Unapiga kazi sana Bashe maana umepungua sana utadhan unaumwa kumbe kazi tu

Hongera Dkt Samia, Hongera Mhe Bashe Hongera Chama cha Mapinduzi.
 
Mhe Bashe nimewasikia ndugu zangu wakisema mara ya mwisho watu wa kusini kufurahia bei ya zao hilo ni mwaka 2019 wakati Rais Magufuli alipozinunua korosho zote.
Hivi ziliishia wapi
Tukumbuke 2019 ilikuwa ni kuelekea 2020
Na sasa tunaelekea 2025 japo naamini Mama aliboresha hali ya hewa ikasaidia ongezeko la korosho
 
CCM nyie ni wajinga sn, kwamba Samia ndiyo ananua korosho au ni imepanda kwenye soko la dunia?
 
CCM nyie ni wajinga sn, kwamba Samia ndiyo ananua korosho au ni imepanda kwenye soko la dunia?
Tena anakiri kuwa bei imepanda kwasababu ya washindani wetu hawajaingia kwenye msimu wao...then anajenga waswasi kuwa za kwetu zitadoda washindani wetu wakianza msimu....sababu ni nini? Poor quality of our product.
Sasa hapo sifa inatoka wapi?
 
Tena anakiri kuwa bei imepanda kwasababu ya washindani wetu hawajaingia kwenye msimu wao...then anajenga waswasi kuwa za kwetu zitadoda washindani wetu wakianza msimu....sababu ni nini? Poor quality of our product.
Sasa hapo sifa inatoka wapi?
Nchi ina watu wapumbavu sn ndiyo maana hatuendelei
 
Sawa muwe na nidhamu ya hela sasa acheni ushamba na matumizi ya kimbwiga, mkiishiwa mnaanza kulialia
Alafu eleweni uchaguzi uko around the corner lazima mpozwee

Ova
Korosho imepanda kwenye soko la dunia wala Samia hana impact yoyote zaidi ya utapeli wa CCM
 
Back
Top Bottom