MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,802
“ Wasafi Tv wanajutia kosa, wameomba msamaha na kuonesha nia ya kusimamia yasijirudie, Wizara inaendelea na jitihada za kuona hili linapata mwelekeo utakaolinda ajira zilizozalishwa, uwekezaji uliofanyika bila kuvunja sheria za Nchi"-Waziri wa Habari Innocent Bashungwa
Taarifa: Darmpya Blog
Taarifa: Darmpya Blog
Hatimaye Waziri wa Habari Mh Bashungwa ameanza mchakato wa kuifungulia Wasafi TV iliyofungiwa na TCRA kwa utovu wa maadili baada ya kumruhusu anayejiita Giggy Money mtoto wa Lisalisa kucheza bila nguo kwenye tamasha lao .
Wiki iliyopita TCRA iliifungia WASAFI TV kwa miezi 6 .
Sababu za mchakato huo zilizotolewa na Bashungwa hazina mashiko kwa vile vyombo vyote vilivyofungiwa na TCRA ikiwemo Kwanza Tv , Gazeti la MwanaHalisi , Mawio na TanzaniaDaima vilikuwa vimeajiri wafanyakazi kama ilivyofanya WASAFI TV lakini vimefungiwa moja kwa moja hadi sasa .
Ni vema Waziri akaweka wazi kwamba amepokea Amri kutoka mahali pengine ili kuifungulia Wasafi TV kwa vile ni wadau wa kampeni zilizododa za ccm kwenye uchaguzi mkuu wa 2020 , ikumbukwe kwamba Diamond Platnums ndiye alikuwa anaendesha kampeni za ccm huku chama chake kikikosa sera za kuwaambia wananchi baada ya kuendelelea kuwa masikini wa kutupwa kwa miaka 60 , hii ni kwa sababu aliyeshindwa jambo kwa muda mrefu wa miaka 60 hawezi kulitatua jambo lilelile kwa miaka mitano .