Waziri Innocent Bashungwa: Wasafi TV wanajutia kosa, wameomba msamaha na kuonesha nia ya kusimamia yasijirudie


Kuita mchakato haramu ni kwa mtazamo wako tu nafikiri....uzito wa kosa pia unaangaliwa

Huwezi fananisha gazeti kama la mwanahalisi lililokuwa linagusa sehemu nyeti sana ukafananisha wa Wasafi tv ambayo kazi kubwa ni burudani hakuna ishu nyingine.

Vitu vingine inatakiwa utumie tu uelewa wa kawaida kuvichanganua, kama we ni mchambuzi wa mambo basi huwezi nambia kuwa utakuwa mgeni kwamba mara nyingi media zinazokuwa zinaandika mambo ya kuikosoa serikali huwa zinakumbana na mkono wa chuma na hii ipo kwenye nchi karibu zote.

Wasafi wale ni burudani tu hata wakifunguliwa hawana madhara
 
Kama hakuwa uchi nini sababu ya kugungiwa wasaf tv?
Ushamba +rohombaya + kuzaliwa vijijini+uzoba=kutulazimisha maisha ambayo kizazi cha SASA hakiyajui........ni sawa na useme kulikuwa na mgao WA maindi ya yanga taifa miaka hiyo....kijana WA SASA hata ajui hayo Mambo na hata akijua inamsaidia nini🤣🤣🤣🤣chefuuuuuuuuu
 

Kwahiyo jambo likiwa karibu kila nchi, linahalalishwa hapa nchini pia? Kwahiyo unaunga mkono uonevu ili serikali isisemwe ama? Kama wasafi wamefungiwa adhabu yao isimame kwa muda stahiki, vinginevyo itakuwa serikali haifanyi kwa uadilifu bali uonevu.
 
Hii haijawahi tokea. Nakumbuka hata kipindi kile Redio Iman ile ya waislam ya Morogoro ilitumikia kipindi chote cha adhabu sikuwahi kusikia utetezi uchwara kama huu.
 
Wangefungiwa tu washike adabu. Tv gani huwezi angalia na wanao?
 
tusubiri pongezi kwa awamu ya tano kulinda ajira za baba levo
 
Bila shaka walikurupuka tu kutoa adhabu.
 
Una roho mbaya wewee,yani sijui ndo mngepata hayo madaraka mngekua mnawalisha watu sumu.

Nilitegemea ungetoa maoni Kama wengine wakiomba msamaha basi wafikiriwe.lakini ndo kwanza unashabikia waendelee kufungiwa.
Ndo Mana tunasema Bora adui umjuae kulikoa usilolijua.Dhamira ya viongozi wa Chadema na wanachama wao Ni roho mbaya ya visasi visvyo na huruma wakijificha ktk mwamvuli wa utetezi wa wananchi.
Mnaonekana tu humu jukwaani mnavyochangia haswa yakiwakumba majnga watu msiowapenda.
Hamna utu kabisaaaaa.
Nendeni zenu na genge lenu la Kijiji huko
 
Mkuu Chadema inahusikaje na maoni yangu ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…