Waziri Jafo amewasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Viwanda na Biashara 2025/2026

Waziri Jafo amewasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Viwanda na Biashara 2025/2026

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Selemani Jafo amewasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2025/2026 jijini Dodoma leo Mei 14, 2025.

Wabunge wanachangia mjadala wa kupitisha bajeti ya wizara hiyo iliyoomba Sh135.7 bilioni ikiwa na vipaumbele saba. Picha na Edwin Mjwahuzi.


====================================​

Kenneth Nollo: Serikali ipunguze kodi ya simu zinazoleta kutoka nje

​

Mbunge wa Bahi, Kenneth Ernest Nollo ameshauri Serikali kupunguza kodi ya kuingiza simu kutoka nje ya Tanzania ili kuwezesha Watanzania wengi kutumia simu janja kwa kuwa hali hiyo itasaidia ongezeko la Watumiaji wa intaneti.

Awali, Nollo alisema, takwimu za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TCRA) za Machi 2025 zinaonesha kuna laini za simu Milioni 90, watumiaji wa intaneti ni Milioni 49, simu zinazomilikiwa zisizo simu janja ni milioni 56 wakati simu janja ni milioni 24, hali inayoonesha bado matumizi ya intaneti ipo chini.
 
Back
Top Bottom